Monday, December 31, 2012

Kwa heri mwaka 2012!

Zaburi 100 "Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote, mtumikieni Bwana kwa furaha, njooni mbele zake kwa kuimba. Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake,
na tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru, nyuani mwake kwa kusifu; mshukuruni, lihimidini jina lake. Kwa kuwa Bwana ndiye mwema, rehema zake ni za milele, na uaminifu wake vizazi na vizazi"

Unapouaga mwaka 2012, hauna budi kumshukuru mungu kwa matendo mengi na makuu aliyokutendea. Umebarikiwa kwa mambo mengi mwaka unaisha leo na inakupasa kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa baraka zote na hata pale ambapo matarajio yako hayakukamilika. Wapo wengi waliotaka kuiona siku na saa kama hii lakini hawapo na sisi. Jihesabie ya kuwa wewe umepata neema ya pekee kwa kuumaliza mwaka huu salama. Kabla ya kulalamika na kulaumu ya kwamba mwaka huu 2012 haukuwa wa matunda kwako, jiulize ni wangapi ambao walishindia mlo mmoja ili hali wewe unakula mara tatu kwa siku na una kazi inayokuingizia kipato, jiulize wakati unalalamika maisha magumu, kuna mwingine anaomba hata tone la mvua lidondoke apate kukinga kinywa chake kwa sababu tu ya kukosa maji, chakula, malazi n.k? Kuna mambo mengi ambayo Mungu amekuepushia hivyo ni vyema kumrudishia sifa na utukufu yeye. Unapoumaliza huu mwaka 2012, mwombe Mungu msamaha pale ambapo ulisahau kumshukuru alipokubariki. Vilevile akusamehe ili uweze kuwasamehe waliokukosea mwaka 2012 na pia usamehewe na uliowakosea ili kesho uanze ukurasa mpya wa mwaka 2013 na baraka pamoja na furaha tele moyoni. Ukianza mwaka mpya na furaha moyoni, hakika kila jambo utakalolifanya mwaka 2013 litabarikiwa.
Mwenyenzi Mungu akupe hekima na busara ya kutafakari mwaka uliopita na kupanga malengo mapya ya mwaka ujao.
Ubarikiwe!

Wednesday, December 26, 2012

I loove this song!

Everyone needs compassion...

Neno la leo

“2Wakorintho 3:14 ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi wakati lisomwapo Agano la kale, utaji uo huo wakaa, yaani haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo”.

TAFAKARI: Akili ikifungwa mtu haoni ugumu wa dhambi. Kwa maana hiyo huo ni Upofu wa mawazo na hivyo kumfanya mtu ashindwe kufanya maamuzi yoyote.
SALA: Mwenyezi Mungu, nakuja mbele zako nikinyenyekea na kukuomba utakase ufahamu wangu niweze kufikiria na kuyafanya yale yakupendezayo. Katika jina la Yesu naomba na kupokea, Amen.

Saturday, December 22, 2012

HOFU YA MUNGU/BWANA NA UCHAJI WAKATI WA KUTOA SADAKA

Kwa nini Mungu anapima uchaji wakati wa kutoa sadaka. Kwa sababu huwezi ukapima kumcha Mungu wakati Mungu hayuko. Yaani mahali ambapo hakuna uwepo wa Mungu. Kama Mungu umemuacha kanisani ukienda utakuwa na hofu ya Mungu na ukirudi mitaani inatoweka. Ni sawa sawa na umekaa na mtumishi wa Mungu mwenye upako, na mbele yake huwezi tamka maneno mabaya kwa sababu utakuwa unamhofia atakuangaliaje.

Mungu hawezi kupima uchaji wa mtu kwa sadaka kidogo. Kwa sababu kwa kila mtihani mwepesi kinachotafutwa ni chepesi hali kadhalika kwa mtihani mgumu kinachotafutwa ni kigumu.

Hofu ya Mungu ni ile hofu inayoonyesha ya kuwa kumtii Mungu kuna thamani kubwa kuliko thamani ya sadaka. Maana yake obedience ya Ibrahimu aliyoonyesha ina thamani kubwa kwa Ibrahim kuliko thamani ya Isaka kwa Ibrahimu.

Hofu ya pili ni ile unampenda Mungu zaidi kuliko sadaka uliyoambiwa uitoe. Mungu anakuhitaji/ kusukuma utoe sadaka ambayo imeshika moyo wako. Kamsubiri Isaka kafika miaka 25 ndiyo akamuambia amtoe kama sadaka.

Ya tatu ni hofu inayoonyesha ya kwamba Mungu ana nafasi ya kwanza kwako kuliko ile sadaka anayokusukuma uitoe. Kwa mfano Mungu anakubariki na kazi nzuri halafu ile kazi aliyokupa inachukua nafasi ya kwanza kwako. Wengine wanasingizia wana kazi nyingi sana hata muda wa kusali hawana. Ndugu yangu ukiendelea na mwendo huo uwepo wa Mungu unakaa mbali na wewe. Umefunga na kuomba kwa ajili ya kupata hiyo kazi na umepata unaaza kumsahau Mungu. Ni dhahiri kwamba Mungu hawezi kukupeleka hatua nyingine.

Ya nne ni hofu inayoonyesha ya kuwa Mungu anaheshima kwako kuliko sadaka aliyokuagiza utoe.
Ya tano ni hofu inayoonyesha ya kuwa ukipewa ufanye uamuzi wa kubaki na Mungu au kubaki na sadaka utachagua kubaki na Mungu na utaitoa Sadaka. Kama Biblia inavyosema “Bali utafuteni kwanza ufalme na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa”. Manake Ibrahimu alikuwa anaulizwa unataka kubaki na nani Isaka au Mimi? Ibrahimu akasema nakutaka wewe (MUNGU).

Ya sita ni hofu inayoonyesha ya kuwa uchague kati ya kumtegemea Mungu ama sadaka unayotegemea kama future yako.Watu wanadhani kumcha Mungu ni kushika Biblia na kusali kanisani kila siku. Unaweza kumuabudu Mungu unavyotaka lakini akikupitisha kwenye Uchaji utafeli kwa sababu hujui. Biblia inasema wapate kujifunza kumcha Mungu daima. Kwahiyo ni hatua ya kujifunza kila siku. Ni kujiuliza kwamba tegemeo la future yako umeweka wapi? Ni swala la prioritization na kumpa Mungu nafasi yake.

Ya saba hofu ya Mungu inayoonyesha unajali zaidi uhusiano wako na Mungu kuliko uhusiano wako na sadaka anayokusukuma kuitoa. Biblia inasema Mungu ni Mungu mwenye wivu. Hapendi umchangamane na kitu kingine. Kama tulivyosoma awali alimwambia Ibrahimu “Ua hayo mahusiano yako na Isaka ili yasiingilie mahusiano yako na mimi” (Mungu).

Ya nane Ni hofu ya Mungu inayoonyesha ya kuwa gharama za kuto-kuitoa hiyo sadaka ni kubwa kuliko baraka za kubaki na hiyo sadaka.Kwa Mungu, Ibrahimu kumtoa Isaka Yesu akawa released. Ni baraka zaidi kumtoa kuliko kubaki naye. Ndiyo maana ikifika swala la Fungu la kumi wengi wanakwama. Uchaji unapimwa kwenye fungu la kumi. Gharama za kutokutii ni kubwa kwa sababu unapata laana. Ukiona watu wanapata shida kwenye kutoa fungu la kumi ujue Uchaji haupo. Kwenye Biblia hamna NET wala GROSS, Biblia inasema ni KIPATO. So kipato chako ni GROSS. Ukiona mtu anajiuliza hayo maswali uchaji wake umepungua. Wengine wanatoa mshahara tu wa kwanza basi anaaza kutoa sababu ya kwamba pengine ndo anaanza maisha kwa hiyo miezi ijayo ataongeza zaidi. Mungu hana shida na hela. Ni kwa ajili ya msaada wako anacheki Uchaji wako.

UCHAJI ni trigger condition ya Mungu. Kwa mfano wa Ibrahimu, baada ya kufaulu mtihani Mwanzo 22:12 anasema usimnyoshee kijana mkono wako…sasa najua unamcha Mungu kwa sababu hukunizuia mwanao, mwanao wa pekee. Mungu alitaka Ibrahimu ajue kuwa katika list ya warithi wake Ishmaeli hayupo. Ishmaeli alibarikiwa na Mungu moja kwa moja (direct). Amebarikiwa na Mungu nje ya covenant (agano). Mungu anambariki Ibrahimu na uzao wake ndiyo maana Ishmail hayupo. Na hivyo kupelekea kumuita Isaka mwana wa pekee.

Condition ya Baraka ya Mwanzo sura ya 12: inasema, “toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha, nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa na kukubariki”…. Akafika kwa ile nchi zile baraka hazioni. Akasema kwa kuwa umetenda neno hili hukunizuia mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki. So hii trigger condition ya pili inadetermine kiwango cha kubarikiwa kwake katika position aliyoko.

Training ya uchaji iko kwenye utoaji wa sadaka. Watu wanachanganya kuwa sio kwa kila kikubwa ni sadaka. Kuna tofauti ya sadaka na zawadi. Sadaka inaacha shimo ama inatengeneza nafasi kwenye moyo wa mtu. Zawadi haiachi shimo. Na ukitoa kilichokuzidi haijalishi ni kikubwa kiasi gani haijawa sadaka.

KUM 8:18-“Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako kama hivi leo” Utajiri unaopewa ni kwa ajili ya covenant sio kwa ajili yako. Hauji kwa sababu umeenda sana shule.

Kazi yako sio source ya blessing ni channel. Just like Isaka was not a source of blessings bali ni channel. Ibrahimu alipompeleka Isaka, Mungu aliachia baraka zake na za uzao wake. Tusisahau kuwa Mungu humpa mbegu mwenye kupanda.

Nawatakia Christmass njema!

 

Tuesday, December 18, 2012

Neno la leo

“Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni wala si kwa lazima, maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu,” 2Wakorintho 9:7
TAFAKARI:Kwa mfano katika kutoa sadaka, kama tunavyoamini kutoa ni moyo, kwa hiyo Mungu akikutana na moyo wako anaangalia Imani uliyo nayo. Haijalishi umekuja na sadaka kiasi gani bali anaangalia imani yako ya utoaji.
SALA: Mungu baba, ninakiri ya kwamba vyote vilivyopo duniani ni mali yako,ninakushukuru kwa maana umenipa moyo wa kukutolea sadaka. Naomba Bwana uuhidhirishe uwepo wako kwangu, pindi nitoapo sadaka nikutane na wewe. Katika jina la Yesu naomba na kushukuru, Amen.

 

Saturday, December 15, 2012

Kwa nini Mungu alimtaka Ibrahimu amtoe Isaka kama sadaka?

Waeb 11:17-19 Kwa imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee, naam yeye aliyeambiwa, Katika Isaka uzao wako utaitwa, akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata kutoka kuzimu, akampata tena toka huko kwa mfano”  Huu ni utoaji kwa sura ya mtoaji. Biblia inaandika kitu gani kilimsukuma Ibrahimu kutoa sadaka kutoka kwenye sababu ya Ibrahimu.  Mwanzo 22:7-8 “Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa mwanangu. Akasema, tazama moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa? Ibrahimu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja,” Isaka aliuliza hili swali kwa sababu alishawahi kumsindikiza baba yake kutoa sadaka wakiwa na mwana-kondoo. Sasa ameuliza asijerudishwa baadae kumleta mwana –kondoo ili hali anajua safari ni ndefu. Ibrahimu akamwambia Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, maana yake sadaka nitakayotoa itazaa mwana-kondoo.

Kwa jicho la Mungu, alikuwa anataka nini? Mwanzo 22: 1-2 “Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema mimi hapa. Akasema, umchukue mwanao, mwana wako wa pekee umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmoja wapo nitakaokuambia,”
Kwa lile neno “Mungu alimjaribu” tunaweza kusema Mungu alimpa mtihani. Jaribu ni jambo linalokuweka njia Panda ya kufikia uamuzi utii unachoambiwa au usitii. Mtihani ni tukio linalopima uwezo wako wa kustahimili na kuyaweza yaliyoko mbele yako katika ngazi inayofuata ya maisha yako.
Wakati Mungu anamuambia Ibrahimu amtoe Isaka kama sadaka ya kuteketezwa, hakuwa na shida na Isaka. Alikuwa na shida na Ibrahimu. Mungu alimpa Ibrahimu maagizo kutaka kujua kama yuko tayari kwa ngazi inayofuata. Yaani kama yuko tayari kufanya kazi ya Mungu anayotaka afanye. Na halikuwa jambo jepesi kwa Ibrahimu. Somo juu ya mtihani huu lilikuwa nini ? Hapa tumepewa somo Mwanzo 22:12Akasema usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno, kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee”
Mungu alimuambia Ibrahimu sasa najua,ya kwamba wewe ni mcha Mungu. Mungu alikuwa anampa mtihani Ibrahimu kwa njia ya sadaka ili kucheki kiwango chake cha Uchaji (kumcha Bwana). Ni wachache sana wakitoa sadaka wanajifunza uchaji. Wengi wanatoa sadaka kwa kutegemea kupata in return. Mungu akikutana na sadaka yako cha kwanza anaangalia Imani yako.
Mbarikiwe!

Friday, December 14, 2012

Ee Mungu tupe Amani....

Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza. Hunihuisha nafsi yangu; na kunio­ngoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake. Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa ma­baya; kwa maana wewe upo pamoja nami, gongo lako na fimbo yako vyanifariji. Waandaa meza mbele yangu, ma­choni pa watesi wangu. Umenipaka mafuta kichwani pangu, na kikombe changu kinafurika. Hakika wema na fadhili zitanifuata siku zote za maisha yangu; nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. (ZAB 23:1-6).
Tukiwa katika kipindi cha majonzi kutokana na tukio la kusikitisha la jana Ijumaa lililotokea katika shule ya elementary ya Sandy Hook huko Newtown,Connecticut,(USA)ni maswali mengi tunayojiuliza kwa nini mambo haya ya kusikitisha na kutisha yanatokea hasa kwa watoto wa kati ya umri wa miaka 5 na 10. Ni kipindi kigumu hasa kwa wazazi ambao huwa wanawaaga watoto asubuhi wakienda shuleni na wakitegemea kwamba watakuwa salama siku nzima. Watoto wadogo huwa na mategemeo mengi ya maisha ya mbeleni na hasa katika kipindi hiki tunachokaribia sikukuu ya kukumbuka kuzaliwa kwa mwokozi wetu Yesu Kristo. Ni jambo la kusikitisha mategemeo na ndoto zao zilivyokatishwa ghafla na matukio ya duniani ambayo mengi yanasababishwa na kutokuwa na upendo na amani. Pamoja na tukio la jana, bado tunakumbushwa kwamba bwana ndiye mchungaji wetu na atatupitisha katika majaribio mengi ambapo wakati mwingine tulifikiria kukata tamaa. Tuendelee kumtegemea Mwenyezi Mungu naye atatupitisha katika vipindi vyote vigumu na mwisho tutakaa naye milele. Zaidi ya yote, tupendane sisi kwa sisi kama alivyotupenda yeye na pia tuwe na amani.
Kwa kumalizia, tunaomba Mwenyenzi Mungu azifariji na kuzipa nguvu familia za wale wote waliopoteza maisha katika tukio la jana. Pia awapumzishe mahali pema watoto wote na watu wazima waliopoteza maisha yao jana. Zaidi awanyooshee mkono wa uponyaji majeruhi wote kwa uponyaji wa haraka.

 

 

Pass me not O gentle saviour


Thursday, December 13, 2012

Neno la leo

“Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa yako mabaki waliochaguliwa kwa neema. Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena au hapo neema isingekuwa neema.” Warumi 11:5-6
Tafakari: Matendo hayatuokoi bali neema hutuokoa. Mungu pekee ndiye atakayetuokoa na hivyo basi haina budi umkiri na kumwamini ndiyo wokovu unaingia halafu matendo yanafuata.
Sala: Mwenyezi Mungu, nasema asante kwa maana umeniokoa kwa damu ya thamani ya mwana wako Yesu Kristo. Naomba uyatawale maisha yangu, nielekeze katika kujua kuufanyia kazi wokovu wangu ili nipate neema yako. Naomba mapenzi yako yatimizwe katika hilo. Amen
Ubarikiwe!

 

Wednesday, December 12, 2012

Neno la leo


Zab 133:1Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza; Ndugu wakae pamoja kwa umoja
Tafakari: Kama neno linavyosema Mungu anapendezewa na watu wakiishi pamoja kwa upendo na amani.Tunajua ya kwamba umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu. Hivyo hatuna budi kushirikiana kwa kila jambo pale ambapo mwenzako, jirani ama ndugu yako anahitaji uwepo wako.
Sala: Mungu Baba, naomba uniepushe na ndimi zenye kuleta ugomvi, nipe moyo wa kupenda kushirikiana na jamaa zangu ili nikaishi kwa amani na jamii inizungukayo, na zaidi nikikuomba uimarishe upendo kati ya ndugu na ndugu. Naomba hayo kupitia Kristo Yesu, Amen.
Siku njema!
 

Bwana umenichunguza


Monday, December 10, 2012

U raise me up!


Neno la Leo

Zaburi 56:4 “Kwa msaada wa Mungu nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa, Mwenye mwili atanitenda nini”
Tafakari: - Mungu atusaidie kumwamini, kumtegemea na kumwogopa yeye siku zote za uhai wetu.
Sala:- Mwenyezi Mungu tunasema asante kwa kuwa wewe umekuwa kimbilio letu na ngome yetu kila tunapokuhitaji. Tunaomba uzidi kutuongoza na kutuimarisha katika neno lako siku zote tukaishi kwa kukutegemea wewe na kukuamini.  Tunaomba hayo kupitia mwanao mpendwa Yesu Kristo, mpatanishi na mwokozi wetu, Amen.
Mbarikiwe!

Saturday, December 8, 2012

Nini Kinasukuma kutoa Sadaka

Zaburi 110:3 “Watu wako wanajitoa kwa hiari. Kinachowafanya/wavutia watu kutoa sadaka ni nini? Kwa sababu kuna na presence ya Mungu.  Uwepo wa Mungu ukiwapo mahali hakutakuwa na haja ya kukimbizana na watu kuhusu utoaji wa sadaka. Kimbizana na Mungu usikimbizane na wanaotoa sadaka. Ukijipanga na Mungu na anointing ikitolewa Mungu atatenda miujiza.
Kutoka 25:1-2 “Bwana akanena na Musa, akamwambia, waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka, kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu,” Ni wale ambao moyo wao uliwasukuma kutoa sadaka walifanya hivyo. Hakuna aliyelazimishwa bali ni kwa kupenda kwao wenyewe kumtolea Mungu.
Kutoka 35:20-22, 29 “Basi mkutano wote wa wana wa Israeli wakaondoka hapo mbele ya Musa. Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu. Nao wakaja waume kwa wake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini na hazama na pete za muhuri na vikuku, na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa BWANA” Hapa inaonyesha waliotoa sadaka ni wale waliokuwa willing kukutana na Mungu na sio kuwa willing kutoa sadaka. Na WOTE haina maana KILA MTU. Waliotoa sadaka walitoa kwa msukumo na kwa vile walikuwa na Imani ya kukutana na Mungu.
Kama maandiko matakatifu yanavyosema Imani huja kwa kuskia na hivyo basi Imani hujengwa moyoni na sio maskioni. Biblia haisemi kwa kuskia mtu huamini. Warumi 10:10 “Kwa maana moyo wa mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”. Ni kwa moyo tu mtu, huamini na kupata.
Ni hatari sana watu kutoa sadaka kwa kuhimizwa na Mchungaji. Watu watakuwa hawatoi kwa uwepo wa Mungu bali kwa sababu mchungaji kawahimiza. Mungu anaangalia moyoni mwako pale utoapo sadaka. Kama ilivyoelezwa mwanzo pale Musa alivyoagizwa na Mungu ya kwamba awaambie wana wa Israeli wamjengee Mungu hema, wale watu wa Israeli walipata anointing yenye mwaliko toka kwa Mungu. Kisha akasema anawasubiri kwa hema (yaani wale watu tu walioenda kwa hema ndo wanakutana na Mungu).
Mbarikiwe!

Thursday, December 6, 2012

Mstari wa Leo

Waebrania 10:23"Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu"

Shida za duniani zisikufanye ukageuka nyuma na kumwacha Mungu, yeye ameahidi na kwa kuwa ni mwaminifu ni kweli atatenda. Aliahidi atatenda mtumaini yeye.
Ubarikiwe!

Wednesday, December 5, 2012

Mstari wa Leo

Yeremia 33:3 “Niite nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua”
 
Pengine kila mtu anaweza shuhudia ni mstari gani wa Biblia umembariki. Kipekee mstari huu unanibariki sana. Sina budi kusema Mungu ameniitikia nilipomuita na anaendelea kunionyesha mambo mengi ambayo kwa akili zangu nisingeweza kuyafikia. Usichoke kumuomba Mungu na kulisoma neno lake. Wapo baadhi ya watu ambao wanaamini wakitaka kumuona Mungu lazima waongee na watumishi fulani yaani wawe wanapewa maono. Kutaka kumuona Mungu sio lazima umtafute mtumishi fulani akuonyeshe. Mungu yupo kwako kila dakika na kila saa. Muite yeye yu karibu na husikia kila tumuitapo.
Ubarikiwe!

 

Monday, December 3, 2012

Sunday, December 2, 2012

Mwakasege teachings:- Mwaliko wa sadaka toka kwa Mungu


Utoaji wa sadaka ni mwaliko binafsi utokao kwa Mungu ili ukutane nae.  2Wakorintho 9:6-7 “Lakini nasema  neno  hili apandae haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni wala si kwa lazima, maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu,”
 Kwa maana kutoa ni moyo, Mungu  akikutana na moyo wako anaangalia na Imani uliyo nayo. Hajalishi umekuja na sadaka kiasi gani. Mtu mwenye Imani ana uhakika ya kwamba ameona na hivyo basi utoaji wako wa sadaka usiegemee ni kwa jinsi gani umeskia mahubiri bali yale maelekezo uyasikiayo toka kwa Mungu ndani ya moyo wako.
Kum 12:10-14 “Lakini mtakapovuka Yordani na kukaa katika nchi anayowarithisha BWANA, Mungu wenu, akawapeni raha, akiwaokoa na adui zenu pande zote mkakaa salama; (11) wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA.  (12) Nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, ninyi na wana wenu, na binti zenu, na watumishi wenu wanaume na wanawake, na Mlawi aliyemo mlangoni mwenu; kwa kuwa hana sehemu wala urithi kwenu. (13) Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa katika kila mahali upaonapo; (14) bali katika mahali atakapopachagua BWANA katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote nikuamuruyo,”
Kama maandiko yanavyosema hapo juu utoaji wa sadaka ni Mwaliko toka kwa Mungu. Katika utoaji wa sadaka unafuata maelekezo ya Mungu na hii ina maana unatoa kwa Imani. Hutoi sadaka kama unavyotaka wewe bali maelekezo ya Mungu  ndiyo yakuongozayo. Huwezi toa sadaka kwa sababu watu wana shida, lakini msaada unawza toa. Kama mstari wa 13 unakupa onyo kabisa kwamba ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa kila mahali upaonapo. Na mstari wa 14 unaonyesha utoe sadaka mahali ambapo Mungu amekuelekeza.
Ntajuaje kuwa hapa ndo bwana alipochagua?
Pale BWANA alipoamua kulikalisha jina lake ndipo unapotakiwa kutoa sadaka zako. Kama kitabu cha Mathayo 18:20 kinavyosema  “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, name nipo papo hapo katikati yao”. Kama mahali ambapo jina lake halipo basi usitoe sadaka. Kwa maana baadhi ya watu wanapenda kutoa sadaka sehemu ambazo wanaona wanapaswa kutoa. Toa sadaka mahali ambapo uwepo wake umekaa. Mathayo 6:21 “ Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako,”. Unapoenda kutoa sadaka sio kwamba Mungu ana shida nayo bali anataka kukutana na moyo wako. Kama ni Kanisani Mungu atakuonyesha kanisa gani. Na ikumbukwe kwamba Imani huja kwa kuskia na sio kila asikiae ana imani. Muombe Bwana auhidhirishe uwepo wake kwako.
Ni makosa kwa kanisa kufikiri linaweza kutengezea heshima ya Mungu katika jamnii. Ni Mungu pekee ndo anaweza kufanya hivyo. Elia alipoomba akasema na ijulikane leo ya kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya kila kitu sawa sawa na neno lako.
Maneno haya maana yake kuna nguvu za Mungu zinakuweko mahali halafu zinanyamaza, unatakiwa uziactivate.  Kule kunyamaza sio kwamba hazipo.  Na kuactivate/kuziamsha  kwake ni kwa kutoa sadaka kwa kusema na ijulikane leo kwa maana utakutana nae (MUNGU). Sema na Mungu ya kwamba unataka Ijulikane leo unapotoa sadaka.
Mungu nataka ijulikane leo unapotoa sadaka hii. Ukisoma  biblia KUTOKA 25:1-23  kuhusiana na ujenzi wa hema jiulize Mungu alipokuwa anaagiza hii sadaka alikuwa anataka nini? Sio kwamba Mungu alikuwa na shida nayo bali hitaji lake ni kutafuta mahali pa kukaa kama mstari wa nane unavyoonyesha wazi “Nao wanifanyie patakatifu, ili nipate kukaa kati yao”. Kwa maana hiyo hitaji la Mungu katika kutoa sadaka si sadaka bali anatafuta mahali pa kukaa.
 Kwa sababu alikuwa haihitaji (angalia mstari wa 8). Tafuta sababu ya Mungu ya kukuambia utoe sadaka. Hitaji la Mungu katika kutoa sadaka si sadaka bali anatafuta a DWEILLING PLACE yaani mahali pa kukaa! KUTOKA 29:42,43 “itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema ya kukutania mbele ya BWANA; hapo nitakapokutana nanyi, ili ninene na wewe hapo. Nami nitakutana na wana wa Isreaeli hapo, na hiyo hema itafanywa takatifu na utukufu wangu”
Utakatifu/Utakaso is to be set apart for the purpose of God. Utukufu wa Mungu ni uwepo wa Mungu uliofunuliwa. Kama unaamini Mungu anaponya lazima kuwe na manifestation kwenye physical being. Hema ni presence ya Mungu. What sets a person apart is the presence of God. Kwa mfano, Kama mhubiri hana anointing juu yake, akihubiri sehemu yenye anointing huhubiri tofauti na watu kusema Yule mhubiri  mbona kwake hajawahi kuhubiri kama hivi? Ikumbukwe kwamba sio yeye bali ni uwepo wa Mungu umemuwezesha kutoa mafundisho ya kipekee tofauti na akiwa kanisani kwake, sio yeye ni Presence ya God imemuwezesha kutoa mafundisho kama hayo.
Mbarikiwe!
 

 

Friday, November 30, 2012

Mstari wa Leo


Yeremia 31:3
BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam, nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.
Mungu anakupenda ndiyo maana unaishi mpaka leo hii. Upendo wake kwetu sisi hauna kikomo. Naamini ni kwa ajili ya upendo wake kwangu na fadhili zake nyingi zinazonifanya niendelee kuishi mpaka wakati huu. Ukimwamini na kumtumaini yeye hakika utaelewa upendo wake juu yako.

Wednesday, November 28, 2012

Mafundisho ya Mwalimu Mwakasege

So wiki hii nitakuwa natoa vipengele mbali mbali vya mafundisho ya Mchungaji Mwakasege. Napendelea kumuita Mwalimu kwa maana kipaji alicho nacho juu ya ufundishaji hakina mfano. Natumaini kila mmoja ataguswa kwa namna yake.
MIMI NI MUNGU WAKO- katika ulimwengu wa roho miungu yoyote ikitaka kukugusa inapambana na yeye.
MIMI NI BWANA MUNGU WAKO- maana yake wewe ni property yake. Yaani anakumiliki. Israelei ni property ya Mungu when you mess with them you mess with God. Kama gari yako ni mtumba ni yako. Mtu akikuonyooshea kidole it doesn’t change anything, gari inabaki kuwa yako tu.
Mbarikiwe!

 

Sunday, November 25, 2012

Marvelous things!

Pata burudani ya Marvelous song from SDA choir in collabo with Ibada ya Kiswahili Columbus, Ohio. Please click the link below

http://www.youtube.com/watch?v=uqLCULpfD64

JE UNAKUMBUKA KUSHUKURU BAADA YA KUPATA?


Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya bwana, dunia na wote wakao ndani yake (Zaburi 24:1). Mwenyenzi Mungu ametukabidhi mamlaka ya kumiliki vitu vyote vilivyopo duniani, hivyo hatuna budi kumshukuru na kumrudishia yeye sifa.
Mara nyingi watu wanapopata walichoomba kwa Mungu kisha wanasahau kusema asante. Na pengine huweka ahadi kwa Mungu kwamba endapo watajibiwa haja zao basi watatoa kitu fulani ama watafanya jambo fulani kama shukrani kwa Mungu.
Kama ulimuomba Mungu akutimizie kitu chako ama tatizo lako pengine ni kupata mtoto halafu ukaahidi kumtolea sadaka ya pekee Mungu wako basi fanya kama ulivyoahidi pasipo kusahau.
Ahadi unayoweka kwa Mungu ni NADHIRI yako na endapo hujaitimiza Mungu anaihesabia kama dhambi na itakufwatilia maishani mpaka hapo utakapotimiza.
Lakini kuna wale wachache wanakumbuka kusema asante na kutoa shukrani zao pindi wapatapo miujiza yao. Mfano mzuri ni ile hadithi ya wenye ukoma kumi,walipopaza sauti na kuita Ee Yesu, Bwana mkubwa uturehemu. Yesu alipowaona akawaambia enendeni mkajionyeshe kwa makuhani na walipokuwa wakienda walitakasika. Na mmoja wao alipoona amepona alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kuu na kuanguka miguuni mwake akamshukuru. Mtu huyu ameshukuru kwa sababu ameuona ukuu wa Mungu, ameguswa kwa namna ya kipekee.(Luka 17:11-19).
Ni mangapi Mungu wetu anatutendea mambo makubwa na mara nyingine tunashangaa miujiza hiyo lakini tunasahau kumshukuru angalau hata kwa kupiga magoti na kusema asante Mungu.
Kama umeweka nadhiri ya kumtolea Mungu sadaka ya shukrani itimize. Labda niseme maana ya Nadhiri nijuavyo mimi ni sadaka uitoayo kwa kinywa chako mwenyewe. Tukumbuke kuwa mara nyingi Nadhiri hutolewa madhabahuni ambapo ni sehemu takatifu.
Madhabahu ni sehemu ambayo inatunza kumbukumbu kwa kila aliyetamka nadhiri yake.Sasa tujiulize tunapotoa nadhiri zetu bila kuzikamilisha hatuogopi madhabahu ama?
Nakumbuka mafundisho ya Mchungaji Christopher Mwakasege juu ya mfano wa wanandoa wawili waliokuwa wanatafuta mtoto kwa muda mrefu bila mafanikio. Wakawa wamezunguka kila sehemu zenye huduma za maombi. Siku moja wakaenda kusali kwa Mchungaji mmoja kimoyo moyo wakasema ‘Mungu ukitupa mtoto tunaahidi kutoa sadaka yetu kwa Mchungaji huyu na kusaidia kanisa lake. Baada ya muda Mungu akawajibu kwa kuwapatia mtoto. Wale wanandoa wakajisahau na kuendelea na maisha yao kama kawaida. Baada ya kipindi kidogo yule mtoto mdogo akaanza kuugua magonjwa mbali mbali hata madaktari wenyewe wasielewe. Ndipo wakamkumbuka Mungu na kuanza kusali.
Mchungaji Mwakasege alifunuliwa na Mungu ya kwamba watu hao walitoa nadhiri mahali fulani na hawajaitimiza, waulize watakuambia wenyewe. Alipowauliza ndipo walipokumbuka ya kwamba hawakutimiza ahadi yao. Wakatubu na kurudi kwenye Kanisa ambapo walipata muujiza na kutubu dhambi zao na kutoa nadhiri yao. Mungu akawasamehe na mtoto akapona.
Huu ni mfano ambao kwangu mimi ulinigusa kwa namna ya pekee. Sijui wewe mwenzangu Mungu amekutendea mangapi na umesahau kumrudishia shukrani.
Kama uliweka nadhiri ya kusaidia ujenzi wa Kanisa mahali ambapo ulipokea muujiza fanya hivyo. Kwa maana wengine hupata muujiza wao sehemu fulani na kwenda kutoa shukrani kanisani kwao walikozoea kusali.
Mwenyenzi Mungu atujalie hekima ya kumshukuru yeye kwa kila jambo!
Mungu awabariki!

 

Friday, November 23, 2012

You hold me now!

No weeping, no hurt or pain, no suffering.... Thank you Jesus for loving me. I will forever be thankful to you.

 

Monday, November 19, 2012

Ujumbe wa Leo

“Angalia, siku zinakuja, asema Bwana Mungu, ambazo nitaleta njaa katika nchi, si njaa ya kukosa chakula, wala kiu ya kukosa maji, bali ya kukosa kuyasikia maneno ya Bwana.” Amosi 8:11
Tumia wakati wako vizuri kumtafakari Mungu na ukuu wake wa ajabu. Kama maandiko yanavyosema hapo juu, kuna wakati utatafuta walau mtu wa kukufundisha neno la Mungu hautapata. Kuna wakati utahitaji huduma za kiroho toka kwa watumishi mbali mbali hautaupata. Tusingojee wakati huo ufike ambapo tutalia na kusaga meno kwa kiu ya kutaka kuskia neno la Mungu. Mtumikie Bwana na tafakari maandiko yake matakatifu nawe utaona raha ya kuishi kwa kumtegemea yeye.
Muwe na Siku njema!

Saturday, November 17, 2012

UPENDO


1 Yohana 4:16"Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake".
Upendo wa Mungu wetu ni mkuu sana na unapita vitu vingi mno. Hata mtu akianza kuandika leo hii juu ya Upendo wa Mungu wino utakwisha kwa maana ni mkubwa mno hauelezeki. Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwana wake wa pekee Yesu Kristo ili kila amwaminie yeye asipotee bali awe na uzima wa milele. Yesu alitufia msalabani kwa ajili ya dhambi zetu, hii inadhihirisha jinsi gani Mungu amempenda mwanae huyo wa pekee afe kwa ajili ya mimi na wewe.
Upendo huleta amani, furaha na faraja. Ndani ya moyo wangu nina amani tele na furaha. Nampenda Kristo kwa sababu ameniokoa kwa damu ya thamani. “Utanijulisha njia ya uzima; mbele za uso wako ziko furaha tele; na katika mkono wako wa kuume mna mema ya milele,” Zaburi 16:11
Upendo hutoka kwa Mungu na kila mwenye upendo ni mtoto wa Mungu. “Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza na akaichukua mioyo yetu kwake mwenyewe” 1 Yohana 4:19. Hakuna kitu muhimu katika maisha ya binadamu kama UPENDO.Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabiri; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote. Upendo haupungui neno wakati wowote - 1Wakorintho 13:4-8
Mtu mwenye kukosa upendo huyo hayuko ndani ya Kristo na siku zote huwa na chuki. Hata katika Biblia imeonyeshwa kwamba mtu akisema anampenda Mungu ana anachukia ndugu yake ni muongo. “1Yohana 4:20 Mtu akisema, nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona”.
Si vyema kuchukiana juu ya mambo madogo madogo.Huna sababu ya kumchukia ndugu yako sababu ya wivu ama kumchukia jirani yako sababu ana maendeleo ambayo wewe huna. Hata amri ya pili inasema mpende jirani yako kama nafsi yako, sasa iweje unamchukia jirani ama ndugu yako wa kuzaliwa naye. Hii haimpendezi Mungu na yakupasa kumrudia yeye na kujifunza neno lake ndipo utaelewa maana halisi ya upendo.  Tuzishike amri za Mungu na kukaa katika pendo lake.
Upendo haujalishi umpendaye ni tajiri ama maskini. Kuna watu ambao huchagua watu wa kuwapenda yaani ambao wanaona wako kwenye status zao. Huo sio upendo bali ni kutafuta watu ambao unadhani utapata furaha kwa sababu tu pengine anaendesha benzi, anakula sehemu za bei ya juu, anavaa vitu vya bei na vitu vingine vinavyofanana na hivyo.
Tuwe na upendo wapendwa kwa sababu ukiwa na upendo siku zote utakua na amani. Kwa maana mtu mwneye Upendo hulipa mabaya kwa mazuri, kamwe hawi wenye visasi. Mwenye upendo siku zote ni mnyenyekevu mbele za watu na hujali wengine zaidi yake mwenyewe.
Usiruhusu mwanadamu akurudishe nyuma na ukatoka katika pendo. Binafsi tangu niijue Biblia maisha yangu yamekuwa ya furaha sana na amani. Na ndiyo maana nasema maisha yangu ni biblia yangu mahali ambapo napata faraja kila nisomapo. Through biblia nimejifunza nini maana halisi ya upendo, na mambo mengine mazuri.
Tujitunze katika upendo wa Mungu, huku tukingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo kwa kutazamia uzima wa milele. Na haya yote yanapatikana kwa kumuomba roho mtakatifu akuongoze uwe na upendo.
Mimi nawapenda, muwe na Jumapili njema.

Thursday, November 15, 2012

Ujumbe wa leo


"Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine. Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu" Wafilipi 2:3-5
Mungu anakupenda ndiyo maana unaishi mpaka leo hii. Mungu wetu hapendezwi na majivuno wala kiburi hupendezwa na wale wenye unyenyekevu. Mungu anatuasa kuacha majivuno na kujiona ni bora kuliko mtu mwingine. Pia anasema tuache kushindana kwa lolote hususan yale tunayoshindania hayana baraka kwake wala hayajengi. Ubinafsi usichukue nafasi ndani ya mioyo yetu, hii itasababisha kututenga mbali na Mungu kwa maana mtu binafsi na mwenye kufanana na mambo kama hayo huhesabiwa maovu na baba yetu wa mbinguni.
Mbarikiwe!

Wednesday, November 14, 2012

Zaburi ya Leo

Zaburi 119: 41-48 "Ee Bwana, fadhili zako zinifikie na mimi, naam wokovu wako sawasawa na ahadi yako. Nami nitamjibu neno anilaumuye, kwa maana nalitumainia neno lako. Usiliondoe neno la kweli kinywani mwangu kamwe, maana nimezingojea hukumu zako. Nami nitaitii sheria yako daima, naam milele na milele. Nami nitakwenda panapo nafasi, kwa kuwa nimejifunza mausia yako. Nitazinena shuhuda zako mbele ya wafalme, wala sitaona aibu. Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako ambayo nimeyapenda. Na mikono yangu nitayainulia maagizo yako niliyoyapenda, nami nitazitafakari amri zako".
Muombe Mungu akupe fadhili zake na udumu katika neno lake. Kwa maana ni neno lake pekee litatuokoa. Songa mbele usisikilize watu wasemayo na siku zote mwanadamu hakosi la kusema. Iwe ni juu ya mafanikio yako ama jambo lolote bado kutakuwa na neno juu yake. Mtumainie Mungu na umuombe sana asiliondoe neno lake kinywani mwako. Zitafakari na kuzifuata amri zake hakika utaona uzuri wa kuishi kwa kumtegemea Mungu.

Mbarikiwe sana!

Sunday, November 11, 2012

Mstari wa Leo


"Kiburi cha mtu kitamshusha, bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa" Mithali 29:23
Mbali na haya maneno ya Biblia juu ya kiburi pia katika maisha ya kawaida kuna methali inasema "kiburi si maungwana". Mtu mwenye kiburi hukosa mengi kwa watu na hata hujikosesha baraka zake toka kwa Mungu. Na ndiyo maana anasema kiburi cha mtu kitamshusha lakini yule mwenye kunyeyekea atapata heshima pamoja na kupata mema.
Unaposoma neno hili kaa utafakari na kama wewe ni mwenye kiburi, jiulize umepata mangapi kutokana na kiburi chako, umekosa mangapi na kimekufikisha wapi? Kumbuka moyo wenye kiburi humchukiza Bwana.
Kiburi hakijifichi, na pengine mwenye kiburi anaweza asione anacho lakini watu wengine wanaweza kutambua kwa haraka kiburi kilichopo ndani ya mtu.
Muombe Mungu akusaidie akuondolee kiburi na akupe moyo wa unyenyekevu upate yaliyo mema. Mara nyingine tunashangaa kwa nini hatuendelei kifedha, kiafya na hata katika mahusiano huoni kilicho cha manufaa, lakini huwezi jua pengine ni kiburi chako hukwamisha hayo yote.

Muwe na wiki yenye kuzaa matunda katika kazi zenu!

FUNGU LA KUMI/ THITHE


Fungu la kumi ni ile asilimia kumi ya mazao ama kipato cha mtu anachopata ambacho anatenga kwa ajili ya kumtolea Mungu.
Kwa kiingereza THITHE is the tenth part of agricultural produce or personal income set apart as an offering to God or for works of mercy, or the same amount regarded as an obligation or tax for the support of the church, priesthood, or the like. OR is a tenth part or any indefinitely small part of anything.
Asilimia 10 ya kipato chako unachotakiwa umtolee Mungu kinatakiwa kiwe kwenye gross salary na sio net salary. Katika hili wapo wenye mtazamo tofauti ya kwamba 10% inatoka kwenye net salary yaani baada ya makato. Binafsi mimi 10% yangu nahesabia kipato changu chote kabla ya makato. Natoa kwa moyo nikijua ya kuwa Mungu pekee ndo atanizidishia. Kumbuka ukitoa extra Mungu nae huona moyo wako ulivyo mkunjufu.
Watu wengi wanapatwa na vishawishi vya kuuliza pindi watoapo fungu lao la kumi ama sadaka zao kuwa zinaenda wapi. Epuka kishawishi cha namna hiyo kwa sababu kinakuzuia kupata baraka za Bwana. Kama utawala wa Kanisa utatumia fungu hilo la kumi kwa kufanya mambo yamchukizayo Mungu, ni juu ya yeye kuwahukumu. Mungu anakujua ya kwamba umemtolea na yeye atakubariki kwa sababu amependezwa na wewe. Kwa kujenga huu msingi wa utoaji fungu la kumi Mungu atakubariki kwenye masuala ya utajiri ambao ni mali, fedha, afya, usalama wako na mambo mengine yanayofanana na hayo. Kwa kifupi utauona mkono wa baraka wa Bwana katika nyanja mbali mbali za maisha yako. Mfano mzuri katika Biblia Kitabu cha Mwanzo 22 ni pale Ibrahimu alipomsikiliza Mungu pale alipotaka amtoe sadaka mwanae wa pekee Isaka. Alipotaka kufanya hivyo akasikia sauti ya Mungu ikimuasa asimtemdee mwanae hivyo kwa maana sasa amejua ya kuwa anamcha Mungu. Ule mstari wa 17 unasema “ katika kubariki nitakubariki na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni na kama mchanga ulioko pwani na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao”
Jenga tabia ya kutoa kwa kuwa utoaji wako unampa Mungu heshima na utukufu. Ni sehemu kubwa ya utukufu. Mtolee Mungu kwa moyo wako wote na sio kutoka kana kwamba unamkopesha Mungu. 2Wakorintho 9:7 “Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala kwa lazima maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu”
Agano la kale linaonyesha kwamba watu walikuwa wakitoa mazao,na wanyama walionona kama fungu la kumi. Kwa ulimwengu wetu wa sasa ambapo watu wengi tumeajiriwa, fungu letu la kumi litahesabiwa kwenye kipato tupatacho katika kazi zetu ama biashara tufanyazo.
Katika kitabu cha Mithali 3:9 “Mheshimu BWANA kwa mali zako na kwa malimbuko ya mazao yako yote, ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika, viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya.”
Pesa kwa sasa imekuwa ngumu na ndiyo maana watu wengine wana mitazamo tofauti ya fungu la kumi. Mtu mwingine anakuambia siwezi toa fungu la kumi kwa sababu sioni likizungumziwa kwenye Agano jipya. Lakini hii ni kutokana na ugumu wa utoaji na upofu wa mtu wa kujua ya kuwa ukimtolea Mungu kazi zako za mikono zinabarikiwa mara dufu. Na pili watu wamekuwa wakiiabudu sana pesa na kusahau kuwa Mungu huyo huyo ndo ametupa uweza wa kutawala vitu kama hivyo.
WAPI NATOA FUNGU LA KUMI
Malaki 3:10 “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo asema Bwana wa majeshi, mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha au la”
Toa fungu lako la kumi nyumbani kwa Bwana ambapo ni mahali unapokwenda kumwabudu yaani Kanisani. Kama umepanga kutoa fungu la kumi litoe hiyo siku uliyopanga, kwa kufanya kinyume chake utakuwa unamuibia Mungu. Kumuibia Mungu maana yake umepanga kutoa fungu lako la kumi kesho halafu inapofika siku ya kutoa unabadili mawazo ama kutoa fungu pungufu, hivyo ni kumuibia Mungu. Mtolee Mungu kwa wakati ulioahidi bila kukoma.
Ninavyoelewa kusaidia wajane, yatima, na wasiojiweza hiyo haihesabiwi kama fungu la kumi, bali inaingia katika upandaji mbegu, yaani kusaidia watu kwa moyo bila kusubiria mrejesho.Nasema hivyo kwa sababu wapo watu wanatoa msaada kwa yatima ama mtu asiyejiweza na kusema hili ndilo fungu langu la kumi. Mmoja wapo ni mimi nilikuwa nasema Mungu niongoze na nifunulie hii pesa nimpe nani ambaye anahitaji zaidi nikijua kuwa ni sehemu yangu ya fungu la kumi bila kujua nilikuwa namuibia Mungu. Kwa hiyo mtu aliyekuwa ananijia kichwani ndiyo nilikuwa nampelekea na kusema kwamba nimetoa fungu la kumi.

KUPANDA MBEGU
Pamoja na kutoa Fungu la kumi, ni vizuri kujenga tabia ya kupanda mbegu yaani kutoa fedha, msaada kwa watu mathalan yatima, wajane na wenye shida mbali mbali kwa nia ya kuvuna mema kutoka kwa Mungu. Kwa kifupi jenga tabia ya kusaidia watu lakini isiwe unafanya mfano kwamba unawekeana mkataba na Mungu ya kuwa ninamsaidia mtu fulani basi lazima Mungu aniongezee. Kwa kufanya hivyo hutafanikiwa kwa sababu unakuwa hujatoa kwa moyo wako wote. Mfano mzuri ni ule na Yesu na mpanzi ( Marko 4:3-8) aliyekwenda kupanda mbegu shambani mwake. Tena kuna hata na wimbo wake. “ Mpanzi alitoka kwenda panda mbegu njema shambani mwake, na nyingine zilianguka kwenye miiba, na nyingne zilianguka pakavu, na nyingine zilianguka kwenye udongo mzurii, zikazaa matunda zikimea na kukua, na kuzaa moja thelathini, moja sitini na moja mia”. Kwa kifupi panda mbegu yako kwenye udongo wenye rutuba, yaani saidia watu wale ambao unajua wanahitaji msaada zaidi kuliko kuwekeza katika miungu mingine.

Maandiko pia yanatuonyesha ya kwamba ni heri kutoa kuliko kupokea (Mdo 20:35). Kwa maana hiyo basi kwa pale unapotoa kwa watu usitegemee kurudishiwa kama ulivyotoa na pengine waweza usirudishiwe kabisa. Jua ya kuwa Mungu ndiyo mpaji, kwa kutoa kwako kwa moyo safi hakika utarudishiwa kwa namna nyingine. Mtolee Mungu kwa moyo wako wote hakika nawe utatimiziwa mahitaji yako. Waebrania 6:14 “Hakika yangu kubariki, nitakubariki na kuongeza nitakuongeza”

Where your treasure is, your heart will be!

 

Wednesday, November 7, 2012

Congrats Mr & Mrs John Adhero

"Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji ya mahali pakavu, nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako na baraka yangu juu yao utakaowazaa" Isaya44:3

Sote wanafamilia tumefurahi kupata habari hizi za ujio wa mgeni Brandon Willness Adhero. Hakika Mungu ni mwema na tutazidi kushangaa matendo yake kwetu sisi hasa ya uumbaji wake. Mungu awatunzie vijana wenu wakue katika misingi ya Kikristo. Awaongoze, awape busara na hekima katika kuwalea na kuwakuza Brandon na kaka yake Austin.
Nasi wanafamilia tunamuomba Mungu nae atuongoze kuwasaidia watoto hawa pale tuwezapo kimawazo katika hatua mbali mbali watakazopitia kimaisha mathalani katika kazi zao za shule na katika kukua kwao katika misingi ya Kristo wetu.
Bwana Mungu awaangazie nuru ya uso wake popote muendapo na katika lolote mfanyalo.
Brandon amezaliwa November 6, 2012!

Monday, November 5, 2012

Such an inspiring message!

Thought I should share this message with you... Hope u will get something out of it!

The song "IT IS WELL WITH MY SOUL" was written by a successful Christian lawyer.He had two girls and a wife, and the family planned a summer trip to go overseas. Since he had a lot of work to do, he sent his family and decided to follow them later. He heard the news while on the following ship that another ship has capsized and he knew that his family was there since they mentioned the name of the ship. On His return home, his Law firm was burned down and the insurance refused to pay, they said "ITS AN ACT OF GOD". He had no money to pay for his house and no work, he also Lost his house. Then while sitting and thinking what's happening to him,being a spiritual person, he wrote a song - whatever my Lord, you have Taught me to say - IT IS WELL, IT IS WELL WITH MY SOUL. My dear friend, a good attitude will determine your altitude. When you look at your life, career, job or family life, what do you say? Do you praise God? Do you blame the devil? A good attitude towards God makes Him move on your behalf. Just sit down & say, Today God , it is well with my soul , I am thankful I had a peaceful sleep , I am thankful I am alive with possibilities , I am thankful I have a roof over me , I am thankful I have a job , I am also thankful that I have Family and Friends. Above All, I AM thankful that I have the lord Jesus Christ on my side.Be blessed. And please don’t be envious or shocked when others are prospering, because you don’t know what they have been through to get there (test, trials and tribulation) so thank God for what you have."Little is much when God is in it IT IS WELL WITH MY SOUL AND YOU?

Saturday, November 3, 2012

UMUHIMU WA KUWA NA MAONO


Kwanza kabisa nianze kwa kutoa maana ya maono ni fikra za kinjozi ama mtu mwenye uwezo wa kuona mbali. Ama ni ile hali ya kitu au tukio lionekanalo kwenye akili lakini kiuhalisia halipo. Kwa lugha ya kizungu naweza kusema a Vision is an experience in which a personage, thing or event appears vividly to the mind although not actually present, often under the influence of a divine or other agency. Simply it is a picture you have in mind that is going to happen.
Ni muhimu kuwa na maono kwa maana maono husaidia mtu ajue anachotaka kufanya na kwa wakati gani. Vile vile ni muhimu kwa sababu maono hutoa taarifa katika maisha ya kila siku ya mwanadamu ni jinsi gani anaweza kuepuka na jambo lolote ama atafanikiwaje kuhusiana na maono yake.
“Pasipo maono watu huacha kujizuia, bali ana heri mtu Yule ashikaye sheria” Mithali 29:18
Maono yako lazima yawe clear tofauti na ndoto. “Wasiuone mwili wake wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosemakwamba yu hai” Luka 24:23. Maono ni yale yanayotabiri mambo yatakayotokea baadae tofauti na ndoto. Mara nyingi ndoto ni accumulation ya mawazo mtu awazayo kwa siku na akilala akaota mambo yafananayo na hayo. Kwa kufanya hivyo hayo si maono, kwa sababu maono yanaweza kutokea wakati wowote iwe mchana ama usingizini.  
Ukiangalia katika kitabu cha Waamuzi mlango wa kumi na tatu pale Malaika wa Bwana alivyomtokea Yule mwanamke tasa na kumwambia atachukua mimba na atamzaa mtoto mwanamume. Ni moja ya mfano wa maono ambayo yako wazi kabisa tofauti na ndoto. “Kwani tazama utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na wembe usipite juu ya kichwa chake maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, naye ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya wafilisti” Waamuzi 13:5
Lakini vile vile ndoto zinaweza kuwa maono mfano mtu anaweza ota anapandishwa cheo lakini wafanyakazi wengine wanapinga jambo hilo na kutaka afukuzwe kazi. Maana ya ndoto kama hiyo jua ya kuwa kuna jambo zuri litatokea katika sehemu yako ya kazi lakini kutakuwa na vipingamizi. Yakupasa kuliombea jambo hilo na kukataa roho hizo za chuki juu ya mafanikio yako.
“Bwana akanijibu akasema, Iandike njozi uifanye wazi sana katika vibao ili aisomaye apate kuisoma kwa maji. Maana njozi hii bado ni wakati ulioamriwa inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake wala haitasema uongo, ijapokawia ingojee kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia” Habakuki 2:2-3

AINA ZA MAONO
·        Personal Vision: Lazima ujue nini unataka katika maisha.Kwa mfano unataka mahusiano yako yaweje iwe umeolewa ama la. What kind of legacy you want your marriage to leave behind? Kwa haraka haraka jiulize mwenyewe nini maono yako kuhusu kipato chako? Pengine unataka uwe mfanyabiashara maarufu ama mkandarasi na hujui jinsi tu ya kufikia malengo yako hayo ya kuwa mfanyabiashara maarufu. Wapo marafiki watakudiscourage kwa kila utakachofanya kwa ajili ya maendeleo yako. Na kama unataka kuendelea never fear about what others will talk about you. Na kama mpaka sasa hujui your personal vision you better find out soon as time is not on your side. Ni muhimu kujua Mungu anataka uwe nani katika maisha yako.

·        Maono ya familia/Family vision: Kwa mfano wewe umeoa/olewa, sasa mkiwa kama mke na mume yaani familia moja ni nini vipaumbele vyenu kwa maisha mapya mliyonayo? Katika tamaduni zetu za kiafrika familia ni muhimu sana. Na kwetu extended families zinapewa umuhimu na hata mara nyingine zinazidi familia za karibu yaani baba, mama, watoto. Na kama mtu utakuwa hujajua jinsi gani ya kuendesha maisha yako kama mtu na mume utajikuta hakuna maendeleo kwa sababu vipaumbele vyako vitakuwa juu ya watu wengine ama nisema ndugu instead of your immediate family.Mfano kuishi nchi za ugenini mathalan US kumefanya sense ya family kupotea na kuanza kuwa individualism. Yaani a family entails Baba, Mama na watoto. Ndugu wengine wanasahaulika huko majumbani na ndiyo maana watu wengine hupata lawama huyu ndugu yetu kabadilika sana hata hasaidii ndugu zake walioko TZ na mambo kama hayo.

Lakini tutambue kwamba Biblia inasema mtu atamuacha Baba na Mama yake ataambatana na mkewe. We should not make our descions basing on what our parents want. Hii haimaanishi kuwa uwadharau unaweza endelea kuwatafuta kwa ushauri lakini jua ya kwamba your immediate family ni mke na watoto wako. Lakini pia hii isiwe sababu ya kukuzuia kusaidia ndugu.

·        Ministry vision:- Unamfanyia nini Mungu? Lazima ujue maono yako katika kumfanyia kazi Mungu. Pengine wewe maono yako ni Mchungaji, ama sister. Ama maono yako wewe ni kusaidia maskini kama Kornelio alivyokuwa anatoa sadaka kwa maskini (soma zaidi Matendo ya mitume 10:9-30). Pia soma Waamuzi 13:2-24 na pia Kitabu cha Daniel kwa ufunuo zaidi juu ya maono.
Mungu awabariki!

Thursday, November 1, 2012

SIKU YA WATAKATIFU

Leo ni sikukuu ya Watakatifu wote. Tunaitumia siku hii kuwakumbuka wapendwa wetu waliotwaliwa na Mwenyezi Mungu. Kipekee namkumbuka Mama yangu mpendwa Mariam Jambia na my little brother Adam. There are times I just wish you are here by my side. I have so many things to share with you Mum. Thank you for shaping me into a person who I like and proud to be. Let me tell you something, you know I'm now married to a wonderful husband most women would wish to have. He is a great person and I thank God for having him. I'm sure if you have had a chance to meet him you would have agreed with all kind of praises about him. On that same day of our wedding, I looked up to see if you can give me a hand in applying my last last make-up before entering the Church. I remember you whispered into my ears, "Kisura wangu I'm not good in make-ups, you know how natural I am". Let me just fix your hair. I felt your hand in my hair and that is when I knew you were besides me all along. Words cannot express how much I miss you dear Mother. You were the greatest thing could have ever happened to me. Not a day goes by without thinking about you especially now when I want to enjoy this good life with you. But I thank God for everything, and I'm proud to be called the daughter of Mariam Jambia. May the almighty God continue to rest your souls in eternal peace.
Also nawakumbuka wakwe zangu Mr & Mrs Willness Lyimo. Always mnakumbukwa na watoto wenu (Jackson, Anitha, Linda, Steve & Manny), wakwe zenu (Dennis, John and Myself), wajukuu (Brianna Lyimo, Austin Adhero, Isaac & Aaron William Rweikiza), ndugu, majirani na marafiki zenu.
My late sis in law Glory Lyimo you were one of a kind. I remember when you were in your A-level studies at Kibosho girls secondary school, I used to admire you so much and your friends sis Maria, Nelly, Chegy and many more. You were full of fun. How ironic life can be, who would have thought I will become one of the members in your family? We live in such a small world, look at me now I'm  called Mrs Jackson Lyimo.
We always pray for you guys and that our living God continue to rest your souls in peace. We love you all and forever will be in our thoughts.
Tunawaombea pia Ndugu, jamaa na marafiki zetu wengine waliotwaliwa na Mungu wapumzike kwa Amani.
Amen!

Tuesday, October 30, 2012

Natembea na Mungu

"Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao na kushika amri zake, hata vizazi elfu." Kum 7:9

Monday, October 29, 2012

Zaburi ya leo

Zaburi 35: 4-5  "Waaibishwe, wafedheheshwe wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma wafadhaishwe wanaonizulia mabaya. Wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa Bwana akiwaangusha chini"

Saturday, October 27, 2012

VIFUNGO VYA LAANA


Neno LAANA katika kamusi limetafsiriwa kama ukosefu wa radhi za mwenyezi Mungu, hasira ya Mungu. Au ni apizo atoalo mtu kwa mtu mwingine ili afikwe na ubaya, uovu, msiba au hasira ya Mungu. LAANI  limetafsiliwa kama, shtakia kwa Mungu, au ombea uovu.

Zipo laana nyingi lakini leo ningependa kuzungumzia laana zifuatazo:-

  1. Ukoo/familia:- laana zinazojiendeleza kwenye ukoo hutokana na matokeo ama matunda ya dhambi. Kwa mfano unakuta katika familia husika kuna wengine wana laana za magonjwa sugu kama kansa, kwenye hiyo hiyo familia wengine hawaolewi, wengine wameolewa lakini ndoa hazidumu, wengine hawapati mimba. Familia nyingine utakuta kuna vifo vya ghafla, wanaanza maisha na kufanikiwa na kuwa na mali na biashara kubwa au kazi lakini mwisho wao wanaishia kufilisika na kufa kwa mateso makali.Unatakiwa kuomba maombi ya rehema na toba na lazima utamke kilichofanyika na matokeo yake.  Kwa sababu kila dhambi iliyofanyika ni kutokana na kuwa na miungu mingine. Dhambi inatokea pale mtu anapomwacha Mungu wa kweli na kusikiliza miungu mingine. Sasa unapokosa msaada wa Mungu wa kweli unapata misaada ya miungu inayokusababisha wewe kutenda kinyume na Mungu. “Usiwe na miungu mingine ila Mimi- Kumbukumbu la torati 5:7”
  2. Laana za kulaaniwa na mtu mwingine:- Yawezekana ulikosana na rafiki yako ama mtu mwingine pengine mwalimu wako wa shule akakuchukia na kukulaani. Anaweza kukulaani kuwa na kamwe hutakaa uendelee kwa kila utakalofanya usifanikiwe.
  3. Laana za kujilaani mwenyewe:- Kuna watu hawaridhiki na jinsi walivyo ama niseme viungo vya miili yao, yaani kwa ufupi hawajikubali ama kujiamini. Utakuta mtu analalamika na kusema “aah mimi kwa ufupi huu sidhani kama nitakaa nipate mwanamke mrefu atakaenipenda, ama mwingine atajilaani kwa kusema kamwe hawezi kuwa mtu wa kwanza darasani kwa sababu tu ya mtu fulani nyumbani kwao hajawahi kuwa” Siku zote maneno huumba na kujiumba, kwa maana hiyo yale uyatamkayo mdomoni kwako vivyo hivyo yanafanyika.
  4. Laana ya vitu visivyoisha: Kuna watu wamelaaniwa kwa kila wakigusacho kisiendelee na matokeo yake hujikuta wameanzisha vitu mbali mbali bila hata kimojawapo kukamilika. Mfano mtu anataka kujenga lakini anaishia nusu na kuanza kitu kingine ambacho nacho hakifiki mbali. Nataka kuanzisha biashara ya nguo, atanunua sehemu ya kuuzia nguo lakini hakuna kitakachoendelea. Watu kama hawa ni wale wanaonena kwa midomo lakini hawatekelezi.
  5.  Laana ya kufanya tendo la ndoa na dada yako au kaka yako, baba yako au mama yako
    Kuna mambo mengine sio rahisi hata kuelezea lakini yapo na yanafanyika mtu amelala na Dada yake, mwingine na kaka yake, laana ya Mungu imeagizwa juu
    yao “Kumb 27:22 Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye au Binti ya mamae. Na watu wote waseme Amina”

Haya yote yanatokana na UPOFU wa mawazo. Akili ikifungwa mtu hawezi kufanya maamuzi yoyote. Pia akili ikifungwa mtu haoni ugumu wa dhambi. “2Wakorintho 3:14 ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi wakati lisomwapo Agano la kale, utaji uo huo wakaa, yaani haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo”. Soma pia Waefeso 4:18

NAVUNJAJE VIFUNGO?
Biblia inapozungumza habari ya watu waliofungwa wapate kufunguliwa, hii ina maana ya kuwa kuna watu wamefungwa chini ya utawala wa nguvu za giza katika ulimwengu wa Roho. Watu hawa wamefungwa kwenye magereza na Ibilisi.
Tutambue ya kuwa Yesu aliposema amekuja kutuokoa hii inamaanisha kwamba kuna mahali ambako tusingeweza kujikwamua wenyewe bila nguvu yake yeye mwenywe kuingia kati yetu.
Aliyahidhirisha haya kwenye kitabu cha nabii Isaya 61:1-2 Roho ya Bwana Mungu i juu yangu kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema, amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao”.
Vunja uhusiano wako na hiyo miungu pamoja na kazi zake na agano lililofanyika kati ya familia au ukoo wako na hiyo miungu. Kila unapotamka mwisho wake sema kwa sababu nimesamehewa. Ipo mistari mingi ya kuvunja maagano lakini mimi nitakupa kifungu hiki cha mstari katika kuvunja maagano na mapoozo ya aina yoyote. “Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa kwa sababu ya kutiwa mafuta” Isaya 10:27
Kifungu kingine ambacho waweza tumia ni kwa kutaja maneno haya wakati wa kuvunja vifungo ama laana “Bwana Yesu, nasimama mbele zako na katika ulimwengu wa roho, kujiachanisha nafsi yangu (Taja jina lako) na vifungo vya kuzimu kwa upande wa baba yangu na mama yangu kwa sababu nimesamehewa.” Endelea vivyo hivyo kwa kutaja, roho na mwili kwa kutumia maneno hayo hayo uponyaji hufanyika katika nafsi, mwili na roho.
Mtegemee Roho Mtakatifu kwa maana atakufundisha mengi ikiwemo kuomba na maagizo ya Yesu. Na kwa kufuata maagizo ya Yesu na kuenenda kwa roho hivyo vifungo vya nafsi vitakwisha. Soma Wagalatia 5:16-25, Luka 22:40-46. Kudumu katika maombi, kuenenda kiroho na kuepuka uovu ni muhimu kwa sababu kwa kufuata misingi hiyo ndipo unafunguliwa vifungo kwa kuombewa ama kwa nguvu inayotenda kazi ndani yako kupitioa roho mtakatifu. Lakini pia ni muhimu kujua ya kwamba sala ya toba pekee haitoshi kumfungua mtu kama ana vifungo na sio imani tu bali na juhudi binafsi ya mtu itasaidia katika kumuweka huru. Wapo watu wanaotaka kupokea miujiza bila ya kuwa na mabadiliko yoyote, ama bila kusoma neno la Mungu na kukua kiroho ama bila kuomba. Wao husubiria siku za maombi, ama mikesha ama makongamano ya maombi ili waombewe kisha baada ya hapo hawajishughulishi katika kukua kiimani.
Kuwa hodari katika Bwana ili upate ulinzi wa Mungu. Waefeso 6:10-11 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani”
Maana ya kuwa hodari katika Bwana ni kukaa kwenye maombi, kusoma na kulishika neno lake liwe ndani yako, na kutaka kumjua yeye zaidi. Sikuzote Sali kwa bidii katika kupambana na muovu shetani ndo mana tunaambiwa vaeni silaha zote za Mungu ili kuweza kupingana na hila za muovu shetani.

Mbarikiwe na Mungu!