Karibuni katika blog hii, mahali ambapo utajifunza kuishi na kuenenda katika njia ya Kikristo na kusaidiana kukua kiroho kwa kusoma na kufundishana neno la Mungu. Ni matumaini yangu kwamba kila mmoja wenu atabarikiwa.
Saturday, October 13, 2012
Ubarikiwe unaposikiliza nyimbo hizi!
Zaburi 135:6 " BWANA amefanya kila lililompendeza, katika mbingu na katika nchi, katika Bahari na katika vilindi vyote"
Wednesday, October 10, 2012
Utajuaje Umesamehe/samehewa
Utajua kuwa jeraha limepona kwa mfano mara ya kwanza ulikuwa
ukimuona ama ukikutana na mtu aliyekukosea mwili unasisimka na unapandwa na
hasira ukitamani ubadilishe njia ama umralue mtu huyo. Lakini ukiongea nae na
kusameheana pindi mkikutana sehemu ama mkionana moyo wako unakuwa una amani na
furaha na mnaongea kawaida, hapo utajua kuwa umepona jeraha lako. Kipimo
kingine cha kujua umemsamehe/ samehewa na mtu uliyekosana nae ni kwamba je maongezi
yenu yanaweza kudumu angalau kwa nusu saa mnaongea na kucheka? Kama hilo
haliwezekani basi jua hujasamehe ama huyu mtu mwingine hajakusamehe.
Mara
nyingine kuna watu wa aina ya kusameheana na mara wanajikuta wanagombana mara
kwa mara. Katika hali kama hiyo endapo wewe umegundua mwenye shida ni mwenzako
na umechoka na hiyo hali ya kukoseana na kusameheana kila wakati basi yakupasa
umuombe Mungu akupe ujasiri wa kusonga mbele.
Kwanza
inabidi ujiulize kwa mfano je nikiacha kujishughulisha na huyu rafiki yangu ni
mangapi napungukiwa? Wakati tukiwa hatupo pamoja ni mangapi nafanya na
kufanikiwa? Na wakati tukiwa hatupo pamoja ni mambo mangapi hayaendi sawa?
Jiulize nitakosa nini kama nitaamua kutojishughulisha nae tena? Lakini hii
haina maana kuwa usisalimiane nae, la hasha unamwambia ukweli kwamba umechoka
na maisha ya namna hiyo cha muhimu kila mtu aendelee na maisha yake lakini bado
tutabaki kuwa marafiki na kusaidiana kwenye shida na raha. Binafsi mimi huu ni
ushauri wangu na nimeona ukifanya kazi kwa baadhi ya watu wa namna hiyo. Cha
muhimu moyo wako uwe umesamehe kweli na una amani kabisa ndani ya moyo wako.
Pengine
umekosana na ndugu yako wa damu na ili hali unajiita mkristo kila siku
unahudhuria Kanisani na unamtolea Mungu sadaka. Lakini kama ndani ya moyo wako
unajua wewe umemkosea ndugu yako hata kama unamcha Mungu kiasi gani unahitaji
neema ya kukuongoza kuombana msamaha na ndugu yako kwa sababu sadaka yako
haipokelewi.
Maandiko
yanatuambia “Basi ukileta sadaka yako madhabahuni na huku ukikumbuka ya
kuwa ndugu yako ana neno juu yako iache sadaka yako mbele ya madhabahu uende
zako, upatane kwanza na ndugu yako kasha urudi uitoe sadaka yako”
Mathayo 5: 23-24
Mind
you, sio kitu kinatokea kwa siku moja, la hasha ni hatua ya muda na inayohitaji
roho mtakatifu akuongoze. Muombe Mungu akupe neema ya Msamaha na neema ya
kudumu ndani ya moyo wako.
Kwa
hiyo tunahitaji kuongozwa sana na roho mtakatifu katika kutoa msamaha na
kujisamehe wenyewe pia.
Sunday, October 7, 2012
Nini kinahitajika katika kuomba msamaha!
Busara (wisdom) inahitajika katika kuomba msamaha ama kukutanishwa na watu mliokosana nao.
Pengine umekosana na mzazi wako ama ndugu yako wa karibu. Mzazi hawezi kumuomba msamaha mtoto wake hata siku moja hata kama anajua yeye ndo mwenye makosa. Unahitaji busara katika kukabiliana na mzazi wako ili kujenga uhusiano wenu tena. Jishushe chini na kumuomba Mungu akupe busara za kwenda kuongea na wazazi wako. Once umefanya hivyo hakika utauona mkono wa Bwana na mambo yako yatakuendea vizuri.
Busara (wisdom) inahitajika katika kuomba msamaha ama kukutanishwa na watu mliokosana nao.
Pengine umekosana na mzazi wako ama ndugu yako wa karibu. Mzazi hawezi kumuomba msamaha mtoto wake hata siku moja hata kama anajua yeye ndo mwenye makosa. Unahitaji busara katika kukabiliana na mzazi wako ili kujenga uhusiano wenu tena. Jishushe chini na kumuomba Mungu akupe busara za kwenda kuongea na wazazi wako. Once umefanya hivyo hakika utauona mkono wa Bwana na mambo yako yatakuendea vizuri.
Je ni vyema kuongelea mambo yaliyopita na mtu mliyekosana
nae baada ya kusameheana?
Jibu la swali hilo ni rahisi tu, inashauriwa kuwa si vyema kukumbushia
mambo ambayo yalikuwa chanzo cha ugomvi kati ya wawili hao. Hiyo inaonyesha
kuwa bado mtu hajaachilia machungu yake. Hivyo basi, kudumu katika amani ni
vyema kutokumbushia mambo ya zamani ama yaliyofanya watu wagombane.
1Wakorintho 13:- Upendo
ndo unaotupelekea kutoa msamaha. Ni kwa ajili ya upendo tu ndiyo nafsi zetu
zitapona. Mstari wa(13) unasema "Basi sasa inadumu imani,
tumaini, upendo, haya matatu na katika hayo lililo kuu ni UPENDO".
Nitaendelea na kipengele cha UTAJUAJE JERAHA LAKO LIMEPONA/UMESAMEHE
Mbarikiwe mpaka mshangae!
Jinsi gani kutokusamehe hupelekea mtu kuwa na uchungu (Bitterness)
Mtu ambae hajaweza kusamehe anakuwa na uchungu ndani ya moyo wake na kuona kila kitu hakiendi kama atakavyo.
Mtu mwenye uchungu ana haya yafuatayo:-
· Yuko negative- Kila kitu kwake kinakuwa ni tofauti
· Mkali-yeye muda wote anafoka na kupayuka
· Hujidharau (put him/herself down)
· Haoni uzuri wa kitu chochote katika maisha ( don’t see any good in life)
· Hatosheki (never satisfied), kila saa atakua analalamika na kutoridhika na kitu chochote.
Kwa maana hiyo sababu tumejua kuwa kutokusamehe huletea mtu kuwa na machungu, sasa basi ni sababu zipi zinazotufanya tuepuke uchungu? (Reasons to avoid bitterness)
·
Uchungu
huharibu mahusiano kati ya Mungu na mwanadamu.
·
Uchungu
unapoteza dira yako
·
Uchungu
unakutenga na watu wengine
·
Uchungu
unakufanya usione uzuri wako na faida yako mwenyewe.
Hayo hapo juu ni mambo ambayo yanatokana na maudhi ambayo
watu wamepitia katika maisha yao. Yamkini mtu alikataliwa wakati akiwa mdogo,
yamkini mzazi wake alimu-abuse (dhalilisha), ama alitelekezwa na mambo mengine
mengine yanayofanania na hayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)