Wednesday, October 3, 2012

Shalom wasomaji wa blog hii. Ni vyema kumshukuru Mungu kwa kutuamsha kila mmoja wetu tukiwa wenye nguvu na afya. Bila kupoteza muda topic ambayo nimeguswa kuizungumzia leo ni suala la MSAMAHA/FORGIVENESS.

Somo la msamaha ni refu mno na ni gumu sana. Lakini hapa kuna vipengele vichache ambavyo vitasaidia walau kuelewa kidogo. Kuna mambo mengine yanatokea miongoni mwa wanadamu mpaka inafikia wakati mtu anakiri kuwa hawezi kusamehe kamwe. Mfano mzuri ni jamii ya wenzetu wa Marekani katika show zao nyingi (reality shows) unakuta mtu ameumizwa pengine kwa kutekelezwa na mzazi wake  ama alikuwa abused wakati alivyokuwa mdogo na hivyo kufikia hatua ya kusema I will never forgive him/her,! Mara nyingi ukiangalia kibinadamu unaweza kusema “hata kama ingekuwa mimi nisingesamehe”. Lakini kwa upande mwingine culture yao ya kuwafanya wawe wazi inasaidia kulikoni jamii kama zetu  (Waafrika) hunyamaza kimya na kuumia na vinyongo vyao.

Kuna watu wamekosewa na kuwakosea wengine. Pia katika hili kuna baadhi ya watu ni wagumu kujishusha na kukubali makosa yao na kuomba msamaha kwa waliowakosea pengine kwa kuhofia kuchekwa. Hii haijalishi hata kidogo, kama nafsi ya mtu imeamua kumsamehe aliyemkosea ni vyema kuomba Mungu akuongoze katika kufanya hivyo. Yawezekana watu hao wawili watajibizana sana kabla ya kuafikiana kuwa wamesameheana lakini hiyo ni moja wapo ya process ya kufanikisha jambo hilo.

 Hata kama mtu uliyemuomba msamaha kakubali kwa kejeli ama la cha msingi Mungu anakuona umesamehe na utapata baraka zako. Kwa sababu vinyongo na kushikilia vitu kwa muda ni mojawapo ya vitu vinavyozuia baraka za watu wengi.

Ikumbukwe kuwa mtu asiposamehe anafukuza baraka zake na siku zote anakuwa amejawa na machungu moyoni mwake. Kuna watu wana magonjwa ya depression, pressure na magonjwa mengine yasiyotambulika. Mara nyingine magonjwa hayo ni matokeo ya machungu mtu aliyo nayo ndani ya nafsi yake. Kila mtu ana past yake na mambo yaliyomtokea. Kama unataka usonge mbele jifunze kusamehe na kuachilia mbali. Kama maelezo ya juu yanavyosema, mwanzo ni vigumu sana sana kusamehe kulingana na makosa.

Muombe Mungu akuponye jeraha lako usamehe, kisha taratibu aendelee kutibu kovu la jeraha lako kwa mtu aliyekukosea. Masomo yanayotuongoza kwenye hili somo la msamaha ni Mathayo 6:14-15, Luka 6:27-29, 37. Mathayo 5:7, 23-24, Marko 11:25, Mathayo 18:21-22, Luka 23:34

Nitaendelea kesho na kipengele cha Jinsi gani kutokusamehe hupelekea mtu kuwa na uchungu (Bitterness)

Neema ya Mungu Baba iwe juu yenu.
 
Hope you will be blessed with this worship song!!!

Tuesday, October 2, 2012

KUMTAFUTA NA KUMWITA MUNGU KWA BIDII


Maandiko matakatifu yanatuasa tuite jina la Bwana Mungu wetu wakati tukiwa kwenye shida na raha. Yeye husikia na hujibu maombi yetu. Imekuwa kawaida kwa wanadamu kumhitaji ama kujisogeza karibu na Mungu wakati wa shida tu. Na mara shida zikiisha humsahau Mungu. Mwanadamu husahau kuwa anatakiwa pia kumuita Mungu akiwa katika raha na mwenye furaha.

Kama maandiko matakatifu yanavyosema Bwana yu karibu na wote wamwitao. Anasema wote wamuitao kwa uaminifu atawafanyia mambo makuu. Sasa basi unamuiteje Mungu? Haijalishi kuwa unajua kusali ama la, kwa maana watu wengi wana mashaka kuwa si rahisi kumuita Mungu kwa kutaja tu jina lake akaskia. MUNGU ANASKIA NA KUJIBU HATA KABLA HUJAMUAMBIA SHIDA YAKO. Kuita kwa kutaja jina lake YESU! YESU! YESU! Inatosha kabisa, waweza kusema ASANTE YESU na yeye anasikia.  Soma Zaburi 145: 18-19 ikuongoze katika hili.

Mungu anasema “Niite name nitakuonyesha mambo makubwa na magumu usiyoyajua” (Yeremia 33:3) Yamkini umepitia katika mapito mengi na mambo magumu ambayo yanakufanya uogope na kuwa njia panda usijue la kufanya, yeye anaweza yote. Mwite na atakuitikia. Ukuu wake ni wa ajabu na matendo yake mengi hushangaza watu.
Jifunze kutumia muda wa faragha na unene na Mungu. Mueleze shida zako na hali zako za namna tofauti unazopitia naye atakuwa pamoja nawe. Soma Isaya 58: 9 ikuongoze katika hili.
Vifungu vingine vya Biblia ambavyo vinatuongoza katika kujua kumuita Mungu ni Mathayo 7:8, Wathesalonike 5:17 na Soma Yohana yote kwa ufunuo zaidi. Ni lazima kujifunze kuomba bila kukoma na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Hakika Mungu ni mwema kwa sisi wanadamu.
Mbarikiwe mpaka mshangae!