Somo la msamaha ni refu mno na ni gumu sana. Lakini hapa
kuna vipengele vichache ambavyo vitasaidia walau kuelewa kidogo. Kuna mambo
mengine yanatokea miongoni mwa wanadamu mpaka inafikia wakati mtu anakiri kuwa
hawezi kusamehe kamwe. Mfano mzuri ni jamii ya wenzetu wa Marekani katika show
zao nyingi (reality shows) unakuta mtu ameumizwa pengine kwa kutekelezwa na
mzazi wake ama alikuwa abused wakati
alivyokuwa mdogo na hivyo kufikia hatua ya kusema I will never forgive him/her,! Mara nyingi ukiangalia kibinadamu
unaweza kusema “hata kama ingekuwa mimi
nisingesamehe”. Lakini kwa upande mwingine culture yao ya kuwafanya wawe
wazi inasaidia kulikoni jamii kama zetu
(Waafrika) hunyamaza kimya na kuumia na vinyongo vyao.
Kuna watu wamekosewa na kuwakosea wengine. Pia katika hili
kuna baadhi ya watu ni wagumu kujishusha na kukubali makosa yao na kuomba
msamaha kwa waliowakosea pengine kwa kuhofia kuchekwa. Hii haijalishi hata
kidogo, kama nafsi ya mtu imeamua kumsamehe aliyemkosea ni vyema kuomba Mungu
akuongoze katika kufanya hivyo. Yawezekana watu hao wawili watajibizana sana
kabla ya kuafikiana kuwa wamesameheana lakini hiyo ni moja wapo ya process ya
kufanikisha jambo hilo.
Hata kama mtu
uliyemuomba msamaha kakubali kwa kejeli ama la cha msingi Mungu anakuona
umesamehe na utapata baraka zako. Kwa sababu vinyongo na kushikilia vitu kwa
muda ni mojawapo ya vitu vinavyozuia baraka za watu wengi.
Ikumbukwe kuwa mtu asiposamehe anafukuza baraka zake na siku
zote anakuwa amejawa na machungu moyoni mwake. Kuna watu wana magonjwa ya
depression, pressure na magonjwa mengine yasiyotambulika. Mara nyingine
magonjwa hayo ni matokeo ya machungu mtu aliyo nayo ndani ya nafsi yake. Kila
mtu ana past yake na mambo yaliyomtokea. Kama unataka usonge mbele jifunze
kusamehe na kuachilia mbali. Kama maelezo ya juu yanavyosema, mwanzo ni vigumu sana
sana kusamehe kulingana na makosa.
Muombe Mungu akuponye jeraha lako usamehe, kisha taratibu
aendelee kutibu kovu la jeraha lako kwa mtu aliyekukosea. Masomo yanayotuongoza kwenye hili somo la msamaha ni Mathayo 6:14-15, Luka 6:27-29, 37. Mathayo 5:7, 23-24, Marko 11:25, Mathayo 18:21-22,
Luka 23:34
Nitaendelea kesho na kipengele cha Jinsi gani kutokusamehe hupelekea mtu kuwa na uchungu (Bitterness)
Neema ya Mungu Baba iwe juu yenu.
Aaameen you too Barikiwa sana dear
ReplyDelete