Saturday, December 22, 2012

HOFU YA MUNGU/BWANA NA UCHAJI WAKATI WA KUTOA SADAKA

Kwa nini Mungu anapima uchaji wakati wa kutoa sadaka. Kwa sababu huwezi ukapima kumcha Mungu wakati Mungu hayuko. Yaani mahali ambapo hakuna uwepo wa Mungu. Kama Mungu umemuacha kanisani ukienda utakuwa na hofu ya Mungu na ukirudi mitaani inatoweka. Ni sawa sawa na umekaa na mtumishi wa Mungu mwenye upako, na mbele yake huwezi tamka maneno mabaya kwa sababu utakuwa unamhofia atakuangaliaje.

Mungu hawezi kupima uchaji wa mtu kwa sadaka kidogo. Kwa sababu kwa kila mtihani mwepesi kinachotafutwa ni chepesi hali kadhalika kwa mtihani mgumu kinachotafutwa ni kigumu.

Hofu ya Mungu ni ile hofu inayoonyesha ya kuwa kumtii Mungu kuna thamani kubwa kuliko thamani ya sadaka. Maana yake obedience ya Ibrahimu aliyoonyesha ina thamani kubwa kwa Ibrahim kuliko thamani ya Isaka kwa Ibrahimu.

Hofu ya pili ni ile unampenda Mungu zaidi kuliko sadaka uliyoambiwa uitoe. Mungu anakuhitaji/ kusukuma utoe sadaka ambayo imeshika moyo wako. Kamsubiri Isaka kafika miaka 25 ndiyo akamuambia amtoe kama sadaka.

Ya tatu ni hofu inayoonyesha ya kwamba Mungu ana nafasi ya kwanza kwako kuliko ile sadaka anayokusukuma uitoe. Kwa mfano Mungu anakubariki na kazi nzuri halafu ile kazi aliyokupa inachukua nafasi ya kwanza kwako. Wengine wanasingizia wana kazi nyingi sana hata muda wa kusali hawana. Ndugu yangu ukiendelea na mwendo huo uwepo wa Mungu unakaa mbali na wewe. Umefunga na kuomba kwa ajili ya kupata hiyo kazi na umepata unaaza kumsahau Mungu. Ni dhahiri kwamba Mungu hawezi kukupeleka hatua nyingine.

Ya nne ni hofu inayoonyesha ya kuwa Mungu anaheshima kwako kuliko sadaka aliyokuagiza utoe.
Ya tano ni hofu inayoonyesha ya kuwa ukipewa ufanye uamuzi wa kubaki na Mungu au kubaki na sadaka utachagua kubaki na Mungu na utaitoa Sadaka. Kama Biblia inavyosema “Bali utafuteni kwanza ufalme na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa”. Manake Ibrahimu alikuwa anaulizwa unataka kubaki na nani Isaka au Mimi? Ibrahimu akasema nakutaka wewe (MUNGU).

Ya sita ni hofu inayoonyesha ya kuwa uchague kati ya kumtegemea Mungu ama sadaka unayotegemea kama future yako.Watu wanadhani kumcha Mungu ni kushika Biblia na kusali kanisani kila siku. Unaweza kumuabudu Mungu unavyotaka lakini akikupitisha kwenye Uchaji utafeli kwa sababu hujui. Biblia inasema wapate kujifunza kumcha Mungu daima. Kwahiyo ni hatua ya kujifunza kila siku. Ni kujiuliza kwamba tegemeo la future yako umeweka wapi? Ni swala la prioritization na kumpa Mungu nafasi yake.

Ya saba hofu ya Mungu inayoonyesha unajali zaidi uhusiano wako na Mungu kuliko uhusiano wako na sadaka anayokusukuma kuitoa. Biblia inasema Mungu ni Mungu mwenye wivu. Hapendi umchangamane na kitu kingine. Kama tulivyosoma awali alimwambia Ibrahimu “Ua hayo mahusiano yako na Isaka ili yasiingilie mahusiano yako na mimi” (Mungu).

Ya nane Ni hofu ya Mungu inayoonyesha ya kuwa gharama za kuto-kuitoa hiyo sadaka ni kubwa kuliko baraka za kubaki na hiyo sadaka.Kwa Mungu, Ibrahimu kumtoa Isaka Yesu akawa released. Ni baraka zaidi kumtoa kuliko kubaki naye. Ndiyo maana ikifika swala la Fungu la kumi wengi wanakwama. Uchaji unapimwa kwenye fungu la kumi. Gharama za kutokutii ni kubwa kwa sababu unapata laana. Ukiona watu wanapata shida kwenye kutoa fungu la kumi ujue Uchaji haupo. Kwenye Biblia hamna NET wala GROSS, Biblia inasema ni KIPATO. So kipato chako ni GROSS. Ukiona mtu anajiuliza hayo maswali uchaji wake umepungua. Wengine wanatoa mshahara tu wa kwanza basi anaaza kutoa sababu ya kwamba pengine ndo anaanza maisha kwa hiyo miezi ijayo ataongeza zaidi. Mungu hana shida na hela. Ni kwa ajili ya msaada wako anacheki Uchaji wako.

UCHAJI ni trigger condition ya Mungu. Kwa mfano wa Ibrahimu, baada ya kufaulu mtihani Mwanzo 22:12 anasema usimnyoshee kijana mkono wako…sasa najua unamcha Mungu kwa sababu hukunizuia mwanao, mwanao wa pekee. Mungu alitaka Ibrahimu ajue kuwa katika list ya warithi wake Ishmaeli hayupo. Ishmaeli alibarikiwa na Mungu moja kwa moja (direct). Amebarikiwa na Mungu nje ya covenant (agano). Mungu anambariki Ibrahimu na uzao wake ndiyo maana Ishmail hayupo. Na hivyo kupelekea kumuita Isaka mwana wa pekee.

Condition ya Baraka ya Mwanzo sura ya 12: inasema, “toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonyesha, nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa na kukubariki”…. Akafika kwa ile nchi zile baraka hazioni. Akasema kwa kuwa umetenda neno hili hukunizuia mwanao wa pekee, katika kubariki nitakubariki. So hii trigger condition ya pili inadetermine kiwango cha kubarikiwa kwake katika position aliyoko.

Training ya uchaji iko kwenye utoaji wa sadaka. Watu wanachanganya kuwa sio kwa kila kikubwa ni sadaka. Kuna tofauti ya sadaka na zawadi. Sadaka inaacha shimo ama inatengeneza nafasi kwenye moyo wa mtu. Zawadi haiachi shimo. Na ukitoa kilichokuzidi haijalishi ni kikubwa kiasi gani haijawa sadaka.

KUM 8:18-“Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako kama hivi leo” Utajiri unaopewa ni kwa ajili ya covenant sio kwa ajili yako. Hauji kwa sababu umeenda sana shule.

Kazi yako sio source ya blessing ni channel. Just like Isaka was not a source of blessings bali ni channel. Ibrahimu alipompeleka Isaka, Mungu aliachia baraka zake na za uzao wake. Tusisahau kuwa Mungu humpa mbegu mwenye kupanda.

Nawatakia Christmass njema!

 

Tuesday, December 18, 2012

Neno la leo

“Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni wala si kwa lazima, maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu,” 2Wakorintho 9:7
TAFAKARI:Kwa mfano katika kutoa sadaka, kama tunavyoamini kutoa ni moyo, kwa hiyo Mungu akikutana na moyo wako anaangalia Imani uliyo nayo. Haijalishi umekuja na sadaka kiasi gani bali anaangalia imani yako ya utoaji.
SALA: Mungu baba, ninakiri ya kwamba vyote vilivyopo duniani ni mali yako,ninakushukuru kwa maana umenipa moyo wa kukutolea sadaka. Naomba Bwana uuhidhirishe uwepo wako kwangu, pindi nitoapo sadaka nikutane na wewe. Katika jina la Yesu naomba na kushukuru, Amen.