Friday, November 30, 2012

Mstari wa Leo


Yeremia 31:3
BWANA alinitokea zamani, akisema, Naam, nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.
Mungu anakupenda ndiyo maana unaishi mpaka leo hii. Upendo wake kwetu sisi hauna kikomo. Naamini ni kwa ajili ya upendo wake kwangu na fadhili zake nyingi zinazonifanya niendelee kuishi mpaka wakati huu. Ukimwamini na kumtumaini yeye hakika utaelewa upendo wake juu yako.

Wednesday, November 28, 2012

Mafundisho ya Mwalimu Mwakasege

So wiki hii nitakuwa natoa vipengele mbali mbali vya mafundisho ya Mchungaji Mwakasege. Napendelea kumuita Mwalimu kwa maana kipaji alicho nacho juu ya ufundishaji hakina mfano. Natumaini kila mmoja ataguswa kwa namna yake.
MIMI NI MUNGU WAKO- katika ulimwengu wa roho miungu yoyote ikitaka kukugusa inapambana na yeye.
MIMI NI BWANA MUNGU WAKO- maana yake wewe ni property yake. Yaani anakumiliki. Israelei ni property ya Mungu when you mess with them you mess with God. Kama gari yako ni mtumba ni yako. Mtu akikuonyooshea kidole it doesn’t change anything, gari inabaki kuwa yako tu.
Mbarikiwe!

 

Sunday, November 25, 2012

Marvelous things!

Pata burudani ya Marvelous song from SDA choir in collabo with Ibada ya Kiswahili Columbus, Ohio. Please click the link below

http://www.youtube.com/watch?v=uqLCULpfD64

JE UNAKUMBUKA KUSHUKURU BAADA YA KUPATA?


Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya bwana, dunia na wote wakao ndani yake (Zaburi 24:1). Mwenyenzi Mungu ametukabidhi mamlaka ya kumiliki vitu vyote vilivyopo duniani, hivyo hatuna budi kumshukuru na kumrudishia yeye sifa.
Mara nyingi watu wanapopata walichoomba kwa Mungu kisha wanasahau kusema asante. Na pengine huweka ahadi kwa Mungu kwamba endapo watajibiwa haja zao basi watatoa kitu fulani ama watafanya jambo fulani kama shukrani kwa Mungu.
Kama ulimuomba Mungu akutimizie kitu chako ama tatizo lako pengine ni kupata mtoto halafu ukaahidi kumtolea sadaka ya pekee Mungu wako basi fanya kama ulivyoahidi pasipo kusahau.
Ahadi unayoweka kwa Mungu ni NADHIRI yako na endapo hujaitimiza Mungu anaihesabia kama dhambi na itakufwatilia maishani mpaka hapo utakapotimiza.
Lakini kuna wale wachache wanakumbuka kusema asante na kutoa shukrani zao pindi wapatapo miujiza yao. Mfano mzuri ni ile hadithi ya wenye ukoma kumi,walipopaza sauti na kuita Ee Yesu, Bwana mkubwa uturehemu. Yesu alipowaona akawaambia enendeni mkajionyeshe kwa makuhani na walipokuwa wakienda walitakasika. Na mmoja wao alipoona amepona alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kuu na kuanguka miguuni mwake akamshukuru. Mtu huyu ameshukuru kwa sababu ameuona ukuu wa Mungu, ameguswa kwa namna ya kipekee.(Luka 17:11-19).
Ni mangapi Mungu wetu anatutendea mambo makubwa na mara nyingine tunashangaa miujiza hiyo lakini tunasahau kumshukuru angalau hata kwa kupiga magoti na kusema asante Mungu.
Kama umeweka nadhiri ya kumtolea Mungu sadaka ya shukrani itimize. Labda niseme maana ya Nadhiri nijuavyo mimi ni sadaka uitoayo kwa kinywa chako mwenyewe. Tukumbuke kuwa mara nyingi Nadhiri hutolewa madhabahuni ambapo ni sehemu takatifu.
Madhabahu ni sehemu ambayo inatunza kumbukumbu kwa kila aliyetamka nadhiri yake.Sasa tujiulize tunapotoa nadhiri zetu bila kuzikamilisha hatuogopi madhabahu ama?
Nakumbuka mafundisho ya Mchungaji Christopher Mwakasege juu ya mfano wa wanandoa wawili waliokuwa wanatafuta mtoto kwa muda mrefu bila mafanikio. Wakawa wamezunguka kila sehemu zenye huduma za maombi. Siku moja wakaenda kusali kwa Mchungaji mmoja kimoyo moyo wakasema ‘Mungu ukitupa mtoto tunaahidi kutoa sadaka yetu kwa Mchungaji huyu na kusaidia kanisa lake. Baada ya muda Mungu akawajibu kwa kuwapatia mtoto. Wale wanandoa wakajisahau na kuendelea na maisha yao kama kawaida. Baada ya kipindi kidogo yule mtoto mdogo akaanza kuugua magonjwa mbali mbali hata madaktari wenyewe wasielewe. Ndipo wakamkumbuka Mungu na kuanza kusali.
Mchungaji Mwakasege alifunuliwa na Mungu ya kwamba watu hao walitoa nadhiri mahali fulani na hawajaitimiza, waulize watakuambia wenyewe. Alipowauliza ndipo walipokumbuka ya kwamba hawakutimiza ahadi yao. Wakatubu na kurudi kwenye Kanisa ambapo walipata muujiza na kutubu dhambi zao na kutoa nadhiri yao. Mungu akawasamehe na mtoto akapona.
Huu ni mfano ambao kwangu mimi ulinigusa kwa namna ya pekee. Sijui wewe mwenzangu Mungu amekutendea mangapi na umesahau kumrudishia shukrani.
Kama uliweka nadhiri ya kusaidia ujenzi wa Kanisa mahali ambapo ulipokea muujiza fanya hivyo. Kwa maana wengine hupata muujiza wao sehemu fulani na kwenda kutoa shukrani kanisani kwao walikozoea kusali.
Mwenyenzi Mungu atujalie hekima ya kumshukuru yeye kwa kila jambo!
Mungu awabariki!