Monday, June 24, 2013

Neno la Leo


Mat 21:22 “Na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea”

TAFAKARI: Jambo la muhimu la kujiuliza hapa ni kwamba unaamini? Unaamini ya kwamba Bwana Mungu yupo na pindi tumuombapo kitu chochote hutupatia?

SALA: Bwana nakiri ya kwamba naamini uwepo wako na ninajua ya kuwa nikiomba unanijibu sawasawa na mapenzi yako. Hata pale ambapo ninatambulika kwa kukosa kujiamini, ninachoomba kutoka kwako ni muongozo, busara na amani katika mambo nifanyayo. Unaniongezea Imani Bwana, pale unapojibu sala zangu. Naomba mkono wako wa busara na hekima usinipungukie ninapoendelea kukutumaini wewe katika maisha yangu. Katika jina la Yesu Kristo naomba na kupokea, Amen.

Sunday, June 23, 2013

Neno la leo



Zab 32:10 “Naye mtu mwovu ana mapigo mengi, Bali amtumainiye BWANA fadhili zitamzunguka”

TAFAKARI: Asubuhi ya leo, mpe Mungu heshima, sifa, heshima, adhama kwa maana yeye anastahili vyote hivyo.Tumtumainiye Mungu katika maisha yetu siku zote, tukiwa kwenye raha ama shida.

SALA: Mwenyezi Mungu, asante kwa kunifanya mtu safi, Bwana najua sijakamilika katika njia zangu lakini wewe umekuwa ukiniangazia nuru ya uso wako siku zote. Naomba usiniache Bwana kwa maana nakuhitaji zaidi katika maisha yangu. Naliinua jina lako na kulibariki kwa maana unastahili sifa. Katika jina la Yesu naomba na kupokea, Amen.