Saturday, December 8, 2012

Nini Kinasukuma kutoa Sadaka

Zaburi 110:3 “Watu wako wanajitoa kwa hiari. Kinachowafanya/wavutia watu kutoa sadaka ni nini? Kwa sababu kuna na presence ya Mungu.  Uwepo wa Mungu ukiwapo mahali hakutakuwa na haja ya kukimbizana na watu kuhusu utoaji wa sadaka. Kimbizana na Mungu usikimbizane na wanaotoa sadaka. Ukijipanga na Mungu na anointing ikitolewa Mungu atatenda miujiza.
Kutoka 25:1-2 “Bwana akanena na Musa, akamwambia, waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka, kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu,” Ni wale ambao moyo wao uliwasukuma kutoa sadaka walifanya hivyo. Hakuna aliyelazimishwa bali ni kwa kupenda kwao wenyewe kumtolea Mungu.
Kutoka 35:20-22, 29 “Basi mkutano wote wa wana wa Israeli wakaondoka hapo mbele ya Musa. Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu. Nao wakaja waume kwa wake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini na hazama na pete za muhuri na vikuku, na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa BWANA” Hapa inaonyesha waliotoa sadaka ni wale waliokuwa willing kukutana na Mungu na sio kuwa willing kutoa sadaka. Na WOTE haina maana KILA MTU. Waliotoa sadaka walitoa kwa msukumo na kwa vile walikuwa na Imani ya kukutana na Mungu.
Kama maandiko matakatifu yanavyosema Imani huja kwa kuskia na hivyo basi Imani hujengwa moyoni na sio maskioni. Biblia haisemi kwa kuskia mtu huamini. Warumi 10:10 “Kwa maana moyo wa mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu”. Ni kwa moyo tu mtu, huamini na kupata.
Ni hatari sana watu kutoa sadaka kwa kuhimizwa na Mchungaji. Watu watakuwa hawatoi kwa uwepo wa Mungu bali kwa sababu mchungaji kawahimiza. Mungu anaangalia moyoni mwako pale utoapo sadaka. Kama ilivyoelezwa mwanzo pale Musa alivyoagizwa na Mungu ya kwamba awaambie wana wa Israeli wamjengee Mungu hema, wale watu wa Israeli walipata anointing yenye mwaliko toka kwa Mungu. Kisha akasema anawasubiri kwa hema (yaani wale watu tu walioenda kwa hema ndo wanakutana na Mungu).
Mbarikiwe!

Thursday, December 6, 2012

Mstari wa Leo

Waebrania 10:23"Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke; maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu"

Shida za duniani zisikufanye ukageuka nyuma na kumwacha Mungu, yeye ameahidi na kwa kuwa ni mwaminifu ni kweli atatenda. Aliahidi atatenda mtumaini yeye.
Ubarikiwe!

Wednesday, December 5, 2012

Mstari wa Leo

Yeremia 33:3 “Niite nami nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua”
 
Pengine kila mtu anaweza shuhudia ni mstari gani wa Biblia umembariki. Kipekee mstari huu unanibariki sana. Sina budi kusema Mungu ameniitikia nilipomuita na anaendelea kunionyesha mambo mengi ambayo kwa akili zangu nisingeweza kuyafikia. Usichoke kumuomba Mungu na kulisoma neno lake. Wapo baadhi ya watu ambao wanaamini wakitaka kumuona Mungu lazima waongee na watumishi fulani yaani wawe wanapewa maono. Kutaka kumuona Mungu sio lazima umtafute mtumishi fulani akuonyeshe. Mungu yupo kwako kila dakika na kila saa. Muite yeye yu karibu na husikia kila tumuitapo.
Ubarikiwe!

 

Sunday, December 2, 2012

Mwakasege teachings:- Mwaliko wa sadaka toka kwa Mungu


Utoaji wa sadaka ni mwaliko binafsi utokao kwa Mungu ili ukutane nae.  2Wakorintho 9:6-7 “Lakini nasema  neno  hili apandae haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni wala si kwa lazima, maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu,”
 Kwa maana kutoa ni moyo, Mungu  akikutana na moyo wako anaangalia na Imani uliyo nayo. Hajalishi umekuja na sadaka kiasi gani. Mtu mwenye Imani ana uhakika ya kwamba ameona na hivyo basi utoaji wako wa sadaka usiegemee ni kwa jinsi gani umeskia mahubiri bali yale maelekezo uyasikiayo toka kwa Mungu ndani ya moyo wako.
Kum 12:10-14 “Lakini mtakapovuka Yordani na kukaa katika nchi anayowarithisha BWANA, Mungu wenu, akawapeni raha, akiwaokoa na adui zenu pande zote mkakaa salama; (11) wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA.  (12) Nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, ninyi na wana wenu, na binti zenu, na watumishi wenu wanaume na wanawake, na Mlawi aliyemo mlangoni mwenu; kwa kuwa hana sehemu wala urithi kwenu. (13) Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa katika kila mahali upaonapo; (14) bali katika mahali atakapopachagua BWANA katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote nikuamuruyo,”
Kama maandiko yanavyosema hapo juu utoaji wa sadaka ni Mwaliko toka kwa Mungu. Katika utoaji wa sadaka unafuata maelekezo ya Mungu na hii ina maana unatoa kwa Imani. Hutoi sadaka kama unavyotaka wewe bali maelekezo ya Mungu  ndiyo yakuongozayo. Huwezi toa sadaka kwa sababu watu wana shida, lakini msaada unawza toa. Kama mstari wa 13 unakupa onyo kabisa kwamba ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa kila mahali upaonapo. Na mstari wa 14 unaonyesha utoe sadaka mahali ambapo Mungu amekuelekeza.
Ntajuaje kuwa hapa ndo bwana alipochagua?
Pale BWANA alipoamua kulikalisha jina lake ndipo unapotakiwa kutoa sadaka zako. Kama kitabu cha Mathayo 18:20 kinavyosema  “Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, name nipo papo hapo katikati yao”. Kama mahali ambapo jina lake halipo basi usitoe sadaka. Kwa maana baadhi ya watu wanapenda kutoa sadaka sehemu ambazo wanaona wanapaswa kutoa. Toa sadaka mahali ambapo uwepo wake umekaa. Mathayo 6:21 “ Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako,”. Unapoenda kutoa sadaka sio kwamba Mungu ana shida nayo bali anataka kukutana na moyo wako. Kama ni Kanisani Mungu atakuonyesha kanisa gani. Na ikumbukwe kwamba Imani huja kwa kuskia na sio kila asikiae ana imani. Muombe Bwana auhidhirishe uwepo wake kwako.
Ni makosa kwa kanisa kufikiri linaweza kutengezea heshima ya Mungu katika jamnii. Ni Mungu pekee ndo anaweza kufanya hivyo. Elia alipoomba akasema na ijulikane leo ya kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya kila kitu sawa sawa na neno lako.
Maneno haya maana yake kuna nguvu za Mungu zinakuweko mahali halafu zinanyamaza, unatakiwa uziactivate.  Kule kunyamaza sio kwamba hazipo.  Na kuactivate/kuziamsha  kwake ni kwa kutoa sadaka kwa kusema na ijulikane leo kwa maana utakutana nae (MUNGU). Sema na Mungu ya kwamba unataka Ijulikane leo unapotoa sadaka.
Mungu nataka ijulikane leo unapotoa sadaka hii. Ukisoma  biblia KUTOKA 25:1-23  kuhusiana na ujenzi wa hema jiulize Mungu alipokuwa anaagiza hii sadaka alikuwa anataka nini? Sio kwamba Mungu alikuwa na shida nayo bali hitaji lake ni kutafuta mahali pa kukaa kama mstari wa nane unavyoonyesha wazi “Nao wanifanyie patakatifu, ili nipate kukaa kati yao”. Kwa maana hiyo hitaji la Mungu katika kutoa sadaka si sadaka bali anatafuta mahali pa kukaa.
 Kwa sababu alikuwa haihitaji (angalia mstari wa 8). Tafuta sababu ya Mungu ya kukuambia utoe sadaka. Hitaji la Mungu katika kutoa sadaka si sadaka bali anatafuta a DWEILLING PLACE yaani mahali pa kukaa! KUTOKA 29:42,43 “itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema ya kukutania mbele ya BWANA; hapo nitakapokutana nanyi, ili ninene na wewe hapo. Nami nitakutana na wana wa Isreaeli hapo, na hiyo hema itafanywa takatifu na utukufu wangu”
Utakatifu/Utakaso is to be set apart for the purpose of God. Utukufu wa Mungu ni uwepo wa Mungu uliofunuliwa. Kama unaamini Mungu anaponya lazima kuwe na manifestation kwenye physical being. Hema ni presence ya Mungu. What sets a person apart is the presence of God. Kwa mfano, Kama mhubiri hana anointing juu yake, akihubiri sehemu yenye anointing huhubiri tofauti na watu kusema Yule mhubiri  mbona kwake hajawahi kuhubiri kama hivi? Ikumbukwe kwamba sio yeye bali ni uwepo wa Mungu umemuwezesha kutoa mafundisho ya kipekee tofauti na akiwa kanisani kwake, sio yeye ni Presence ya God imemuwezesha kutoa mafundisho kama hayo.
Mbarikiwe!