Wafilipi 2:12
“Basi, wapendwa wangu kama vile mlivyotii sikuzote si wakati mimi nilipokuwa
tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa
kuogopa na kutetemeka”
TAFAKARI: Maandiko matakatifu
yanatuasa kuutimiza wokovu wetu kwa kuogopa na kutetemeka. Tudumu katika neno
lake na kuzitii amri zake ili tuweze kusimama imara katika imani yetu ya
wokovu. Na zaidi tuepuke kulitumia neno la wokovu kwa kuficha mambo yetu
mabaya. Katika kufanya haya yatupasa kujitwika msalaba wake na kuwa mfuasi wake
na kufanya yale yampendezayo. Vile vile kutambua eneo lako kama mkristo ni lipi
ambalo litakufanya utimize wokovu wako.
SALA: Bwana Yesu, tunakuja mbele
zako kwa unyeyekevu kabisa tukiomba utujalie maskio ya kuskia na kudumu katika
neno lako. Tuwezeshe kuutambua wokovu wetu na kuushika tusiterereke kamwe.
Zaidi tusaidie kuwa mfano wa wafuasi wako tukiubeba msalaba wako kwa imani na
ya kwamba ipo siku tutafurahia matunda ya wokovu wetu. Tunaomba hayo na
kupokea, Amen.