Kutoka 25:1-2 “Bwana
akanena na Musa, akamwambia, waambie wana wa Israeli kwamba wanitwalie sadaka,
kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu,” Ni
wale ambao moyo wao uliwasukuma kutoa sadaka walifanya hivyo. Hakuna
aliyelazimishwa bali ni kwa kupenda kwao wenyewe kumtolea Mungu.
Kutoka 35:20-22, 29 “Basi
mkutano wote wa wana wa Israeli wakaondoka hapo mbele ya Musa. Wakaja kila mtu
ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa
apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania na
kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu. Nao wakaja waume kwa wake,
wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini na hazama na pete za muhuri
na vikuku, na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la
kumpa BWANA” Hapa inaonyesha waliotoa sadaka ni wale waliokuwa willing
kukutana na Mungu na sio kuwa willing kutoa sadaka. Na WOTE haina maana KILA
MTU. Waliotoa sadaka walitoa kwa msukumo na kwa vile walikuwa na Imani ya
kukutana na Mungu.
Kama maandiko matakatifu yanavyosema Imani huja kwa kuskia na
hivyo basi Imani hujengwa moyoni na sio maskioni. Biblia haisemi kwa kuskia mtu
huamini. Warumi 10:10 “Kwa maana moyo wa mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri
hata kupata wokovu”. Ni kwa moyo tu mtu, huamini na kupata.
Ni hatari sana watu kutoa sadaka kwa kuhimizwa na Mchungaji.
Watu watakuwa hawatoi kwa uwepo wa Mungu bali kwa sababu mchungaji kawahimiza.
Mungu anaangalia moyoni mwako pale utoapo sadaka. Kama ilivyoelezwa mwanzo pale
Musa alivyoagizwa na Mungu ya kwamba awaambie wana wa Israeli wamjengee Mungu
hema, wale watu wa Israeli walipata anointing yenye mwaliko toka kwa Mungu.
Kisha akasema anawasubiri kwa hema (yaani wale watu tu walioenda kwa hema ndo
wanakutana na Mungu).
Mbarikiwe!
No comments:
Post a Comment