Utoaji wa sadaka ni mwaliko binafsi utokao kwa Mungu ili ukutane
nae. 2Wakorintho
9:6-7 “Lakini nasema neno hili apandae haba atavuna haba; apandaye kwa
ukarimu atavuna ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si
kwa huzuni wala si kwa lazima, maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa
ukunjufu,”
Kwa maana kutoa ni moyo,
Mungu akikutana na moyo wako anaangalia na Imani uliyo
nayo. Hajalishi umekuja na sadaka kiasi gani. Mtu mwenye Imani ana uhakika ya
kwamba ameona na hivyo basi utoaji wako wa sadaka usiegemee ni kwa jinsi gani
umeskia mahubiri bali yale maelekezo uyasikiayo toka kwa Mungu ndani ya moyo
wako.
Kum 12:10-14 “Lakini mtakapovuka Yordani
na kukaa katika nchi anayowarithisha BWANA, Mungu wenu, akawapeni raha,
akiwaokoa na adui zenu pande zote mkakaa salama; (11) wakati huo itakuwa kwamba
mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo
mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu
zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote
teule mtakazoweka kwa BWANA. (12) Nanyi
mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, ninyi na wana wenu, na binti zenu, na
watumishi wenu wanaume na wanawake, na Mlawi aliyemo mlangoni mwenu; kwa kuwa
hana sehemu wala urithi kwenu. (13) Ujihadhari usitoe sadaka zako za
kuteketezwa katika kila mahali upaonapo; (14) bali katika mahali
atakapopachagua BWANA katika kabila zako mojawapo, ndipo utakapotoa sadaka zako
za kuteketezwa, ndipo utakapotenda yote nikuamuruyo,”
Kama maandiko yanavyosema hapo juu utoaji wa sadaka ni Mwaliko
toka kwa Mungu. Katika utoaji wa sadaka unafuata maelekezo ya Mungu na hii ina
maana unatoa kwa Imani. Hutoi sadaka kama unavyotaka wewe bali maelekezo ya
Mungu ndiyo yakuongozayo. Huwezi toa
sadaka kwa sababu watu wana shida, lakini msaada unawza toa. Kama mstari wa 13
unakupa onyo kabisa kwamba ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa kila
mahali upaonapo. Na mstari wa 14 unaonyesha utoe sadaka mahali ambapo Mungu
amekuelekeza.
Ntajuaje
kuwa hapa ndo bwana alipochagua?
Pale BWANA alipoamua kulikalisha jina lake ndipo unapotakiwa
kutoa sadaka zako. Kama kitabu cha Mathayo 18:20
kinavyosema “Kwa kuwa walipo wawili
watatu wamekusanyika kwa jina langu, name nipo papo hapo katikati yao”.
Kama mahali ambapo jina lake halipo basi usitoe sadaka. Kwa maana baadhi ya
watu wanapenda kutoa sadaka sehemu ambazo wanaona wanapaswa kutoa. Toa sadaka
mahali ambapo uwepo wake umekaa. Mathayo 6:21 “ Kwa
kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako,”. Unapoenda
kutoa sadaka sio kwamba Mungu ana shida nayo bali anataka kukutana na moyo
wako. Kama ni Kanisani Mungu atakuonyesha kanisa gani. Na ikumbukwe kwamba
Imani huja kwa kuskia na sio kila asikiae ana imani. Muombe Bwana auhidhirishe
uwepo wake kwako.
Ni makosa kwa kanisa kufikiri linaweza kutengezea heshima ya
Mungu katika jamnii. Ni Mungu pekee ndo anaweza kufanya hivyo. Elia alipoomba
akasema na ijulikane leo ya kwamba mimi ni mtumishi wako na nimefanya kila kitu
sawa sawa na neno lako.
Maneno haya maana yake kuna nguvu za Mungu zinakuweko mahali
halafu zinanyamaza, unatakiwa uziactivate. Kule kunyamaza sio kwamba hazipo. Na kuactivate/kuziamsha kwake ni kwa kutoa sadaka kwa kusema na ijulikane
leo kwa maana utakutana nae (MUNGU). Sema na Mungu ya kwamba unataka Ijulikane
leo unapotoa sadaka.
Mungu nataka ijulikane leo unapotoa sadaka hii. Ukisoma biblia KUTOKA 25:1-23 kuhusiana na ujenzi wa hema jiulize Mungu
alipokuwa anaagiza hii sadaka alikuwa anataka nini? Sio kwamba Mungu alikuwa na
shida nayo bali hitaji lake ni kutafuta mahali pa kukaa kama mstari wa nane
unavyoonyesha wazi “Nao wanifanyie patakatifu, ili
nipate kukaa kati yao”. Kwa maana hiyo hitaji la Mungu katika kutoa
sadaka si sadaka bali anatafuta mahali pa kukaa.
Kwa sababu alikuwa
haihitaji (angalia mstari wa 8). Tafuta sababu ya Mungu ya kukuambia utoe
sadaka. Hitaji la Mungu katika kutoa sadaka si sadaka bali anatafuta a
DWEILLING PLACE yaani mahali pa kukaa! KUTOKA 29:42,43 “itakuwa
ni sadaka ya kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema
ya kukutania mbele ya BWANA; hapo nitakapokutana nanyi, ili ninene na wewe
hapo. Nami nitakutana na wana wa Isreaeli hapo, na hiyo hema itafanywa takatifu
na utukufu wangu”
Utakatifu/Utakaso is to be set apart for the purpose of God.
Utukufu wa Mungu ni uwepo wa Mungu uliofunuliwa. Kama unaamini Mungu anaponya
lazima kuwe na manifestation kwenye physical being. Hema ni presence ya Mungu.
What sets a person apart is the presence of God. Kwa mfano, Kama mhubiri hana
anointing juu yake, akihubiri sehemu yenye anointing huhubiri tofauti na watu kusema
Yule mhubiri mbona kwake hajawahi
kuhubiri kama hivi? Ikumbukwe kwamba sio yeye bali ni uwepo wa Mungu
umemuwezesha kutoa mafundisho ya kipekee tofauti na akiwa kanisani kwake, sio
yeye ni Presence ya God imemuwezesha kutoa mafundisho kama hayo.
Mbarikiwe!
No comments:
Post a Comment