Tuesday, October 2, 2012

KUMTAFUTA NA KUMWITA MUNGU KWA BIDII


Maandiko matakatifu yanatuasa tuite jina la Bwana Mungu wetu wakati tukiwa kwenye shida na raha. Yeye husikia na hujibu maombi yetu. Imekuwa kawaida kwa wanadamu kumhitaji ama kujisogeza karibu na Mungu wakati wa shida tu. Na mara shida zikiisha humsahau Mungu. Mwanadamu husahau kuwa anatakiwa pia kumuita Mungu akiwa katika raha na mwenye furaha.

Kama maandiko matakatifu yanavyosema Bwana yu karibu na wote wamwitao. Anasema wote wamuitao kwa uaminifu atawafanyia mambo makuu. Sasa basi unamuiteje Mungu? Haijalishi kuwa unajua kusali ama la, kwa maana watu wengi wana mashaka kuwa si rahisi kumuita Mungu kwa kutaja tu jina lake akaskia. MUNGU ANASKIA NA KUJIBU HATA KABLA HUJAMUAMBIA SHIDA YAKO. Kuita kwa kutaja jina lake YESU! YESU! YESU! Inatosha kabisa, waweza kusema ASANTE YESU na yeye anasikia.  Soma Zaburi 145: 18-19 ikuongoze katika hili.

Mungu anasema “Niite name nitakuonyesha mambo makubwa na magumu usiyoyajua” (Yeremia 33:3) Yamkini umepitia katika mapito mengi na mambo magumu ambayo yanakufanya uogope na kuwa njia panda usijue la kufanya, yeye anaweza yote. Mwite na atakuitikia. Ukuu wake ni wa ajabu na matendo yake mengi hushangaza watu.
Jifunze kutumia muda wa faragha na unene na Mungu. Mueleze shida zako na hali zako za namna tofauti unazopitia naye atakuwa pamoja nawe. Soma Isaya 58: 9 ikuongoze katika hili.
Vifungu vingine vya Biblia ambavyo vinatuongoza katika kujua kumuita Mungu ni Mathayo 7:8, Wathesalonike 5:17 na Soma Yohana yote kwa ufunuo zaidi. Ni lazima kujifunze kuomba bila kukoma na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Hakika Mungu ni mwema kwa sisi wanadamu.
Mbarikiwe mpaka mshangae!

4 comments:

  1. Congrats Sayuni for this wonderful blog I believe it will be a blessing to many people. Those who lost hope will be uplifted for the next level of Glory for the Glory of God. You have inspired me a lot and also uplifted my faith as I read this blog. Be blessed and keep it up God Almighty will bless you as you continue to do his work and will take you to the next level. By Baraka Saiteu-Tanzania.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Thank you so much Baraka! May the good Lord keep on blessing more people who come accross this blog!
      Im glad I inspired you and hope to continue doing so in so many ways!

      Delete
    2. hakika nimebarikiwa sana na somo lako zuri

      Delete