Sunday, October 7, 2012

Nini kinahitajika katika kuomba msamaha!
Busara (wisdom) inahitajika katika kuomba msamaha ama kukutanishwa na watu mliokosana nao.
 
Pengine umekosana na mzazi wako ama ndugu yako wa karibu. Mzazi hawezi kumuomba msamaha mtoto wake hata siku moja hata kama anajua yeye ndo mwenye makosa. Unahitaji busara katika kukabiliana na mzazi wako ili kujenga uhusiano wenu tena. Jishushe chini na kumuomba Mungu akupe busara za kwenda kuongea na wazazi wako. Once umefanya hivyo hakika utauona mkono wa Bwana na mambo yako yatakuendea vizuri.




Je ni vyema kuongelea mambo yaliyopita na mtu mliyekosana nae baada ya kusameheana?

Jibu la swali hilo ni rahisi tu, inashauriwa kuwa si vyema kukumbushia mambo ambayo yalikuwa chanzo cha ugomvi kati ya wawili hao. Hiyo inaonyesha kuwa bado mtu hajaachilia machungu yake. Hivyo basi, kudumu katika amani ni vyema kutokumbushia mambo ya zamani ama yaliyofanya watu wagombane.

1Wakorintho 13:- Upendo ndo unaotupelekea kutoa msamaha. Ni kwa ajili ya upendo tu ndiyo nafsi zetu zitapona.  Mstari wa(13) unasema "Basi sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu na katika hayo lililo kuu ni UPENDO".
Nitaendelea na kipengele cha UTAJUAJE JERAHA LAKO LIMEPONA/UMESAMEHE
Mbarikiwe mpaka mshangae!

1 comment:

  1. i like but can tell out what is mean by Mathayo 28:19 na 20

    ReplyDelete