Sunday, October 7, 2012

 Jinsi gani kutokusamehe hupelekea mtu kuwa na uchungu (Bitterness)



Mtu ambae hajaweza kusamehe anakuwa na uchungu ndani ya moyo wake na kuona kila kitu hakiendi kama atakavyo.

Mtu mwenye uchungu ana haya yafuatayo:-

· Yuko negative- Kila kitu kwake kinakuwa ni tofauti

· Mkali-yeye muda wote anafoka na kupayuka

· Hujidharau (put him/herself down)

· Haoni uzuri wa kitu chochote katika maisha ( don’t see any good in life)

· Hatosheki (never satisfied), kila saa atakua analalamika na kutoridhika na kitu chochote.


 Kwa maana hiyo sababu tumejua kuwa kutokusamehe huletea mtu kuwa na machungu, sasa basi ni sababu zipi zinazotufanya tuepuke uchungu? (Reasons to avoid bitterness)
·         Uchungu huharibu mahusiano kati ya Mungu na mwanadamu.
·         Uchungu unapoteza dira yako
·         Uchungu unakutenga na watu wengine
·         Uchungu unakufanya usione uzuri wako na faida yako mwenyewe.
Hayo hapo juu ni mambo ambayo yanatokana na maudhi ambayo watu wamepitia katika maisha yao. Yamkini mtu alikataliwa wakati akiwa mdogo, yamkini mzazi wake alimu-abuse (dhalilisha), ama alitelekezwa na mambo mengine mengine yanayofanania na hayo.

No comments:

Post a Comment