Kwanza kabisa nianze kwa
kutoa maana ya maono ni fikra za kinjozi ama mtu mwenye uwezo wa kuona mbali.
Ama ni ile hali ya kitu au tukio lionekanalo kwenye akili lakini kiuhalisia
halipo. Kwa lugha ya kizungu naweza kusema a Vision is an experience in which a
personage, thing or event appears vividly to the mind although not actually
present, often under the influence of a divine or other agency. Simply it is a
picture you have in mind that is going to happen.
Ni muhimu kuwa na maono
kwa maana maono husaidia mtu ajue anachotaka kufanya na kwa wakati gani. Vile
vile ni muhimu kwa sababu maono hutoa taarifa katika maisha ya kila siku ya
mwanadamu ni jinsi gani anaweza kuepuka na jambo lolote ama atafanikiwaje
kuhusiana na maono yake.
“Pasipo maono watu huacha
kujizuia, bali ana heri mtu Yule ashikaye sheria” Mithali 29:18
Maono yako lazima yawe clear tofauti
na ndoto. “Wasiuone mwili wake wakaja wakasema ya
kwamba wametokewa na malaika waliosemakwamba yu hai” Luka 24:23. Maono
ni yale yanayotabiri mambo yatakayotokea baadae tofauti na ndoto. Mara nyingi
ndoto ni accumulation ya mawazo mtu awazayo kwa siku na akilala akaota mambo
yafananayo na hayo. Kwa kufanya hivyo hayo si maono, kwa sababu maono yanaweza
kutokea wakati wowote iwe mchana ama usingizini.
Ukiangalia katika kitabu cha Waamuzi
mlango wa kumi na tatu pale Malaika wa Bwana alivyomtokea Yule mwanamke tasa na
kumwambia atachukua mimba na atamzaa mtoto mwanamume. Ni moja ya mfano wa maono
ambayo yako wazi kabisa tofauti na ndoto. “Kwani tazama
utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto mwanamume na wembe usipite juu ya kichwa
chake maana mtoto huyo atakuwa mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, naye ataanza
kuwaokoa Israeli na mikono ya wafilisti” Waamuzi 13:5
Lakini vile vile ndoto zinaweza kuwa
maono mfano mtu anaweza ota anapandishwa cheo lakini wafanyakazi wengine
wanapinga jambo hilo na kutaka afukuzwe kazi. Maana ya ndoto kama hiyo jua ya
kuwa kuna jambo zuri litatokea katika sehemu yako ya kazi lakini kutakuwa na
vipingamizi. Yakupasa kuliombea jambo hilo na kukataa roho hizo za chuki juu ya
mafanikio yako.
“Bwana akanijibu akasema,
Iandike njozi uifanye wazi sana katika vibao ili aisomaye apate kuisoma kwa
maji. Maana njozi hii bado ni wakati ulioamriwa inafanya haraka ili kuufikilia
mwisho wake wala haitasema uongo, ijapokawia ingojee kwa kuwa haina budi kuja,
haitakawia” Habakuki 2:2-3
AINA ZA MAONO
·
Personal
Vision: Lazima ujue nini unataka katika
maisha.Kwa mfano unataka mahusiano yako yaweje iwe umeolewa ama la. What kind
of legacy you want your marriage to leave behind? Kwa haraka haraka jiulize
mwenyewe nini maono yako kuhusu kipato chako? Pengine unataka uwe
mfanyabiashara maarufu ama mkandarasi na hujui jinsi tu ya kufikia malengo yako
hayo ya kuwa mfanyabiashara maarufu. Wapo marafiki watakudiscourage kwa kila
utakachofanya kwa ajili ya maendeleo yako. Na kama unataka kuendelea never fear
about what others will talk about you. Na kama mpaka sasa hujui your personal
vision you better find out soon as time is not on your side. Ni muhimu kujua
Mungu anataka uwe nani katika maisha yako.
·
Maono
ya familia/Family vision: Kwa mfano wewe
umeoa/olewa, sasa mkiwa kama mke na mume yaani familia moja ni nini vipaumbele
vyenu kwa maisha mapya mliyonayo? Katika tamaduni zetu za kiafrika familia ni
muhimu sana. Na kwetu extended families zinapewa umuhimu na hata mara nyingine
zinazidi familia za karibu yaani baba, mama, watoto. Na kama mtu utakuwa
hujajua jinsi gani ya kuendesha maisha yako kama mtu na mume utajikuta hakuna
maendeleo kwa sababu vipaumbele vyako vitakuwa juu ya watu wengine ama nisema
ndugu instead of your immediate family.Mfano kuishi nchi za ugenini mathalan US
kumefanya sense ya family kupotea na kuanza kuwa individualism. Yaani a family
entails Baba, Mama na watoto. Ndugu wengine wanasahaulika huko majumbani na
ndiyo maana watu wengine hupata lawama huyu ndugu yetu kabadilika sana hata
hasaidii ndugu zake walioko TZ na mambo kama hayo.
Lakini tutambue kwamba
Biblia inasema mtu atamuacha Baba na Mama yake ataambatana na mkewe. We should
not make our descions basing on what our parents want. Hii haimaanishi kuwa uwadharau
unaweza endelea kuwatafuta kwa ushauri lakini jua ya kwamba your immediate
family ni mke na watoto wako. Lakini pia hii isiwe sababu ya kukuzuia kusaidia
ndugu.
·
Ministry
vision:- Unamfanyia nini Mungu? Lazima ujue
maono yako katika kumfanyia kazi Mungu. Pengine wewe maono yako ni Mchungaji,
ama sister. Ama maono yako wewe ni kusaidia maskini kama Kornelio alivyokuwa
anatoa sadaka kwa maskini (soma zaidi Matendo ya mitume
10:9-30). Pia soma Waamuzi 13:2-24 na pia Kitabu cha Daniel kwa ufunuo zaidi
juu ya maono.
Mungu awabariki!
Good job Sayuni
ReplyDeleteThank you mpenzi!
ReplyDelete