Fungu la kumi ni
ile asilimia kumi ya mazao ama kipato cha mtu anachopata ambacho anatenga kwa
ajili ya kumtolea Mungu.
Kwa kiingereza
THITHE is the
tenth part of agricultural produce or personal income set apart as an offering
to God or for works of mercy, or the same amount regarded
as an obligation or tax for the support of the
church, priesthood, or the like. OR is a tenth part or any indefinitely small
part of anything.
Asilimia
10 ya kipato chako unachotakiwa umtolee Mungu kinatakiwa kiwe kwenye gross
salary na sio net salary. Katika hili wapo wenye mtazamo tofauti ya kwamba 10%
inatoka kwenye net salary yaani baada ya makato. Binafsi mimi 10% yangu
nahesabia kipato changu chote kabla ya makato. Natoa kwa moyo nikijua ya kuwa
Mungu pekee ndo atanizidishia. Kumbuka ukitoa extra Mungu nae huona moyo wako
ulivyo mkunjufu.
Watu wengi
wanapatwa na vishawishi vya kuuliza pindi watoapo fungu lao la kumi ama sadaka
zao kuwa zinaenda wapi. Epuka kishawishi cha namna hiyo kwa sababu kinakuzuia
kupata baraka za Bwana. Kama utawala wa Kanisa utatumia fungu hilo la kumi kwa
kufanya mambo yamchukizayo Mungu, ni juu ya yeye kuwahukumu. Mungu anakujua ya
kwamba umemtolea na yeye atakubariki kwa sababu amependezwa na wewe. Kwa
kujenga huu msingi wa utoaji fungu la kumi Mungu atakubariki kwenye masuala ya
utajiri ambao ni mali, fedha, afya, usalama wako na mambo mengine yanayofanana
na hayo. Kwa kifupi utauona mkono wa baraka wa Bwana katika nyanja mbali mbali za
maisha yako. Mfano mzuri katika Biblia Kitabu cha Mwanzo 22 ni pale Ibrahimu
alipomsikiliza Mungu pale alipotaka amtoe sadaka mwanae wa pekee Isaka.
Alipotaka kufanya hivyo akasikia sauti ya Mungu ikimuasa asimtemdee mwanae
hivyo kwa maana sasa amejua ya kuwa anamcha Mungu. Ule mstari wa 17 unasema “ katika kubariki
nitakubariki na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni
na kama mchanga ulioko pwani na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao”
Jenga tabia ya kutoa kwa kuwa
utoaji wako unampa Mungu heshima na utukufu. Ni sehemu kubwa ya utukufu. Mtolee
Mungu kwa moyo wako wote na sio kutoka kana kwamba unamkopesha Mungu. 2Wakorintho 9:7 “Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni
mwake, si kwa huzuni, wala kwa lazima maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo
wa ukunjufu”
Agano la kale
linaonyesha kwamba watu walikuwa wakitoa mazao,na wanyama walionona kama fungu
la kumi. Kwa ulimwengu wetu wa sasa ambapo watu wengi tumeajiriwa, fungu letu
la kumi litahesabiwa kwenye kipato tupatacho katika kazi zetu ama biashara
tufanyazo.
Katika kitabu cha Mithali 3:9 “Mheshimu BWANA kwa mali zako na kwa malimbuko ya
mazao yako yote, ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika, viriba vyako
vitafurika kwa mvinyo mpya.”
Pesa kwa sasa imekuwa ngumu na
ndiyo maana watu wengine wana mitazamo tofauti ya fungu la kumi. Mtu mwingine
anakuambia siwezi toa fungu la kumi kwa sababu sioni likizungumziwa kwenye
Agano jipya. Lakini hii ni kutokana na ugumu wa utoaji na upofu wa mtu wa kujua
ya kuwa ukimtolea Mungu kazi zako za mikono zinabarikiwa mara dufu. Na pili
watu wamekuwa wakiiabudu sana pesa na kusahau kuwa Mungu huyo huyo ndo ametupa
uweza wa kutawala vitu kama hivyo.
WAPI NATOA FUNGU LA KUMI
Malaki 3:10 “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba
yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo asema Bwana wa majeshi, mjue kama
sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo
nafasi ya kutosha au la”
Toa fungu lako la kumi nyumbani
kwa Bwana ambapo ni mahali unapokwenda kumwabudu yaani Kanisani. Kama umepanga
kutoa fungu la kumi litoe hiyo siku uliyopanga, kwa kufanya kinyume chake
utakuwa unamuibia Mungu. Kumuibia Mungu maana yake umepanga kutoa fungu lako la
kumi kesho halafu inapofika siku ya kutoa unabadili mawazo ama kutoa fungu
pungufu, hivyo ni kumuibia Mungu. Mtolee Mungu kwa wakati ulioahidi bila
kukoma.
Ninavyoelewa kusaidia wajane,
yatima, na wasiojiweza hiyo haihesabiwi kama fungu la kumi, bali inaingia
katika upandaji mbegu, yaani kusaidia watu kwa moyo bila kusubiria mrejesho.Nasema
hivyo kwa sababu wapo watu wanatoa msaada kwa yatima ama mtu asiyejiweza na
kusema hili ndilo fungu langu la kumi. Mmoja wapo ni mimi nilikuwa nasema Mungu
niongoze na nifunulie hii pesa nimpe nani ambaye anahitaji zaidi nikijua kuwa
ni sehemu yangu ya fungu la kumi bila kujua nilikuwa namuibia Mungu. Kwa hiyo
mtu aliyekuwa ananijia kichwani ndiyo nilikuwa nampelekea na kusema kwamba
nimetoa fungu la kumi.
KUPANDA MBEGU
Pamoja na kutoa
Fungu la kumi, ni vizuri kujenga tabia ya kupanda mbegu yaani kutoa fedha, msaada
kwa watu mathalan yatima, wajane na wenye shida mbali mbali kwa nia ya kuvuna
mema kutoka kwa Mungu. Kwa kifupi jenga tabia ya kusaidia watu lakini isiwe
unafanya mfano kwamba unawekeana mkataba na Mungu ya kuwa ninamsaidia mtu
fulani basi lazima Mungu aniongezee. Kwa kufanya hivyo hutafanikiwa kwa sababu
unakuwa hujatoa kwa moyo wako wote. Mfano mzuri ni ule na Yesu na mpanzi (
Marko 4:3-8) aliyekwenda kupanda mbegu shambani mwake. Tena kuna hata na wimbo
wake. “ Mpanzi alitoka kwenda panda mbegu njema shambani mwake, na nyingine
zilianguka kwenye miiba, na nyingne zilianguka pakavu, na nyingine zilianguka
kwenye udongo mzurii, zikazaa matunda zikimea na kukua, na kuzaa moja
thelathini, moja sitini na moja mia”. Kwa kifupi panda mbegu yako kwenye udongo
wenye rutuba, yaani saidia watu wale ambao unajua wanahitaji msaada zaidi
kuliko kuwekeza katika miungu mingine.
Maandiko pia
yanatuonyesha ya kwamba ni heri kutoa kuliko kupokea (Mdo 20:35). Kwa maana hiyo basi kwa pale unapotoa kwa watu usitegemee
kurudishiwa kama ulivyotoa na pengine waweza usirudishiwe kabisa. Jua ya kuwa
Mungu ndiyo mpaji, kwa kutoa kwako kwa moyo safi hakika utarudishiwa kwa namna
nyingine. Mtolee Mungu kwa moyo wako wote hakika nawe utatimiziwa mahitaji
yako. Waebrania 6:14 “Hakika yangu kubariki,
nitakubariki na kuongeza nitakuongeza”
Where your
treasure is, your heart will be!
No comments:
Post a Comment