Sunday, November 11, 2012

Mstari wa Leo


"Kiburi cha mtu kitamshusha, bali mwenye roho ya unyenyekevu ataheshimiwa" Mithali 29:23
Mbali na haya maneno ya Biblia juu ya kiburi pia katika maisha ya kawaida kuna methali inasema "kiburi si maungwana". Mtu mwenye kiburi hukosa mengi kwa watu na hata hujikosesha baraka zake toka kwa Mungu. Na ndiyo maana anasema kiburi cha mtu kitamshusha lakini yule mwenye kunyeyekea atapata heshima pamoja na kupata mema.
Unaposoma neno hili kaa utafakari na kama wewe ni mwenye kiburi, jiulize umepata mangapi kutokana na kiburi chako, umekosa mangapi na kimekufikisha wapi? Kumbuka moyo wenye kiburi humchukiza Bwana.
Kiburi hakijifichi, na pengine mwenye kiburi anaweza asione anacho lakini watu wengine wanaweza kutambua kwa haraka kiburi kilichopo ndani ya mtu.
Muombe Mungu akusaidie akuondolee kiburi na akupe moyo wa unyenyekevu upate yaliyo mema. Mara nyingine tunashangaa kwa nini hatuendelei kifedha, kiafya na hata katika mahusiano huoni kilicho cha manufaa, lakini huwezi jua pengine ni kiburi chako hukwamisha hayo yote.

Muwe na wiki yenye kuzaa matunda katika kazi zenu!

No comments:

Post a Comment