Lakini kadri mtoto anavyokua na kuendelea kumuomba mzazi wake kitu inafikia
wakati mzazi anachoka na pengine kuanza kulalamika ya kuwa mtoto huyu anaomba sana.
Vivyo hivyo ni sawa na maisha yetu na Mungu baba wa mbinguni.
Naye vile vile huwa anachoka pale kila saa tunapoomba atutimizie mahitaji yetu.
Yoh 1:11-13 “Alikuja kwake wala walio wake hawakumpokea. Bali wote
waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio
jina lake; waliozaliwa si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu”
Anatuambia wale wote waliompokea wamefanyika kuwa watoto wake.
Je unamfurahishaje baba yako wa mbinguni kama umfurahishapo mzazi wako. Waweza
kusema ni kwa kufuata yale atufundishayo na kuendenda katika njia anazotuongoza yeye. Lakini kwa kumfanyia vitu ambavyo yeye atajiskia furaha ya kuwa mwanangu
kafanya haya machoni pangu na imenipendeza.
Ni vyema unapoamka ukamshukuru Mungu kwa kukuamsha salama.
Mwambie asante Mungu kwa kuniamsha salama nikiwa mwenye nguvu na afya tele.
Muulize Mungu nikufanyie nini kwa siku ya leo? Ama nikuimbie nyimbo gani leo? Nikusomee
zaburi gani Bwana? Mueleze ya kwamba unatambua vipaji vingi alivyokupa na
muulize ungependa uwabarikije wengine kwa vipaji hivyo? Nina hakika kwa kufanya
hivyo moyo wako utakua umejawa na furaha na siku yako itakuwa nzuri.
Hata katika maisha ya kawaida si mzazi unafurahia sana pale
mtoto anapokufanyia kitu? Unafurahi kuona mtoto amekupikia, amekununulia zawadi
kwa uwezo wake mwenyewe na mambo mengine yanayofanana na hayo. Hiyo ni mifano
ya kufananisha na maisha ya kumtumikia Mungu wetu.Jenga tabia hiyo ya kuamka na kumuuliza Mungu umfanyie nini badala ya kuamka na kumuomba tu kila siku akusikilize na akusaidie wewe tu. Kwa kufuata haya moyo wako utakusukuma kufanya mambo mengi kwa kuongozwa na roho mtakatifu.
Mbarikiwe!
No comments:
Post a Comment