Waeb
11:17-19 Kwa
imani Ibrahimu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea
hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee, naam yeye aliyeambiwa,
Katika Isaka uzao wako utaitwa, akihesabu ya kuwa Mungu aweza kumfufua hata
kutoka kuzimu, akampata tena toka huko kwa mfano” Huu ni utoaji kwa sura ya mtoaji. Biblia inaandika
kitu gani kilimsukuma Ibrahimu kutoa sadaka kutoka kwenye sababu ya
Ibrahimu. Mwanzo 22:7-8 “Isaka akasema na Ibrahimu baba yake, akinena, Babangu! Naye
akasema, Mimi hapa mwanangu. Akasema, tazama moto upo, na kuni zipo, lakini
yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa? Ibrahimu akasema, Mungu
atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili
pamoja,” Isaka aliuliza hili swali kwa sababu alishawahi kumsindikiza
baba yake kutoa sadaka wakiwa na mwana-kondoo. Sasa ameuliza asijerudishwa
baadae kumleta mwana –kondoo ili hali anajua safari ni ndefu. Ibrahimu
akamwambia Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, maana yake sadaka
nitakayotoa itazaa mwana-kondoo.
Kwa jicho la Mungu, alikuwa anataka nini? Mwanzo 22: 1-2 “Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu,
akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema mimi hapa. Akasema, umchukue mwanao,
mwana wako wa pekee umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe
sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmoja wapo nitakaokuambia,”
Kwa lile neno “Mungu alimjaribu” tunaweza kusema Mungu alimpa
mtihani. Jaribu ni jambo linalokuweka njia Panda ya kufikia uamuzi utii
unachoambiwa au usitii. Mtihani ni tukio linalopima uwezo wako wa kustahimili
na kuyaweza yaliyoko mbele yako katika ngazi inayofuata ya maisha yako.
Wakati Mungu anamuambia Ibrahimu amtoe Isaka kama sadaka ya
kuteketezwa, hakuwa na shida na Isaka. Alikuwa na shida na Ibrahimu. Mungu
alimpa Ibrahimu maagizo kutaka kujua kama yuko tayari kwa ngazi inayofuata.
Yaani kama yuko tayari kufanya kazi ya Mungu anayotaka afanye. Na halikuwa
jambo jepesi kwa Ibrahimu. Somo juu ya mtihani huu lilikuwa nini ? Hapa
tumepewa somo Mwanzo 22:12
“Akasema usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee
neno, kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, iwapo hukunizuilia mwanao,
mwanao wa pekee”
Mungu alimuambia Ibrahimu sasa najua,ya kwamba wewe ni mcha
Mungu. Mungu alikuwa anampa mtihani Ibrahimu kwa njia ya sadaka ili kucheki
kiwango chake cha Uchaji (kumcha Bwana). Ni wachache sana wakitoa sadaka
wanajifunza uchaji. Wengi wanatoa sadaka kwa kutegemea kupata in return. Mungu
akikutana na sadaka yako cha kwanza anaangalia Imani yako.
Mbarikiwe!