Friday, May 10, 2013

Neno la leo

Eze 33:5 “Aliisikia sauti ya tarumbeta, wala hakuonywa; damu yake itakuwa juu yake; lakini kama angalionywa, angalijiokoa roho yake”

TAFAKARI: Pale mtu akifanya uovu humuambii damu yake iko juu yako. Mungu hapendezwi na kifo cha mwovu, hivyo basi ni vyema kusaidia wenzetu pale tunapoona wanahitaji kuokolewa ama kukosolewa. Tusikazane kujiokoa wenyewe na kuwanyooshea vidole wengine, bali turudishe kondoo wa bwana kundini kwa kusaidia kukosoa wale wanaoenenda njia za uovu.
SALA: Mwenyezi Mungu, nakuja mbele zako nikiomba msamaha pale ambapo nimeenda kinyume na mapenzi yako. Bwana mara nyingine nimejifikiria mwenyewe na kusahau kutenda kazi yako. Nifanye niwe mfano wa neno lako kwa kusaidia kuwaonya wale waangukao. Zaidi nipe nguvu za kusimama imara katika kuitenda kazi yako. Naomba katika jina la Yesu Kristo, Amen.

2 comments:

  1. Amen b blssd dear naomba unikimbuke kwenye maombi Roho wa Mungu akuongoze thx.Mrs Simon frm Mwanza

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amen Mrs Simon, nafurahi kuona unabarikiwa na blog hii. Tuzidi kudumu katika maombi, Mungu wetu hasinzii wala halali hakika maombi yetu yatajibiwa kama bado hayajajibiwa. Uzidi kubarikiwa!

      Delete