Pia kuna amri au maagizo ambayo yanahitaji mjadala ambapo ili
zitekelezeke. Kwa mfano amri/agizo zinazowekwa na serikali ni zile amri ambazo
mara nyingi zinahitaji mjadala. Yaani zitakapotolewa mtu atauliza kwa nini
napaswa kutii hii amri? Kisha ataelezwa matokeo ya kutii na kutotii amri hiyo.
Tukija upande wa Baba yetu mbinguni, amri zake na maagizo yake
ni sawa na maagizo au amri atoazo mzazi kwa mtoto wake, yaani hayahitaji mjadala. Kwa maana nyingine amri/
maagizo hayo ni kamilifu.
Ukisoma kitabu cha KUTOKA 20 habari yote inaelezea amri na
maagizo Mungu aliyotoa ambayo ni kamilifu. Mungu wetu ametupa amri kamilifu
kwamba hataki kuchanganywa na kitu chochote kwa maana yeye ni Mungu mwenye
wivu. Mstari wa 5 unasema “Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa
mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba
zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao”
Wapendwa katika kipindi hiki cha Kwaresma, tunapotafakari
kuteswa kwa BWANA wetu Yesu Kristo,
tunatakiwa kuendelea kuzitii amri zake na kufuata maagizo yake bila mjadala
kwani amri zake zimekamilika na ni rahisi kuzifuata. Ni amri ambazo hazina
maswali ya “KWA NINI?”
Mbarikiwe!
No comments:
Post a Comment