TAFAKARI: Neema yake Mungu
imetuwezesha wengi kupata mahitaji yetu. Mara nyingine kulazimisha mambo ili
kupata mahitaji yetu na kusahau kwamba ipo neema kubwa tu juu yetu.
SALA: Bwana, nikitazama maisha
yangu uliyonipa naona baraka zako kubwa. Neema yako imeniruhusu kufikia malengo
yangu. Yapo mambo mengi nataka kufanya lakini nimejifunza kusubiri kwa maana
wewe hujibu kwa wakati wako. Nitoe kutoka kwenye fikra za wivu, hukumu na
uchoyo, kwa sababu nataka kutoshelezwa na neema yako tu pekee. Katika jina la
Yesu naomba na kupokea, Amen.
No comments:
Post a Comment