TAFAKARI: Wakati wa kwaresma ni muda ambao tunakuwa wenye kusafishwa na roho wa Mungu. Ni roho mtakatifu wa Mungu ndiye anaetukusanya pamoja na wote wamfuatao Kristo, ni kama kondoo waliopotea wanaporudishwa zizini hali kadhalika habari za mwana mpotevu nae alipoamua kurudi kwa baba yake. Hivi vyote havikutendeka pasipo kuongozwa na roho wa Mungu.
SALA: Bwana Yesu, tunaomba roho
wako mtakatifu atuongoze ili tuweze kutambua nafasi zetu katika familia na
kutenda yale yanayokupendeza wewe. Katika jina la Yesu tunaomba na kupokea,
Amen.
No comments:
Post a Comment