Wednesday, February 13, 2013

Nawatakia Kwarema njema!

Rum 2:4 " Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu"

TAFAKARI: Hili ni somo zuri kwa ajili ya Jumatano hii ya majivu. Sababu kubwa ya Mungu kukuita kuwa karibu naye ni kutokana na upendo na wema alionao. Mungu anakuita utubu dhambi zako ili uweze kubadilika na kufuata njia mpya katika maisha yako. Katika kipindi hichi cha kwaresma, kutubu inachukua nafasi kubwa sana. Muombe Mungu akusaidie uweze kusamehe na kuwasamehe wale wote waliokukwaza namna yoyote ile.

SALA: Bwana Mungu, wewe mwenye ukarimu na wema wa ajabu, tunaomba utuongoze katika maisha mapya ambayo yanatuelekeza kutubu, ili tukaishi kwa upendo na amani ndani ya mioyo yetu tukijua ya kwamba umetusamehe nasi tumewasamehe waliotukosea, Katika jina la Yesu naomba na kupokea, Amen.

2 comments:

  1. Tunashukuru kwa maneno mazuri ya nayo tiya moyo na kutujenga kiroho.MUNGU azidi kukutia nguvu huzidi kutulisha na kutufundisha maneneo yake.

    ReplyDelete