Karibuni katika blog hii, mahali ambapo utajifunza kuishi na kuenenda katika njia ya Kikristo na kusaidiana kukua kiroho kwa kusoma na kufundishana neno la Mungu. Ni matumaini yangu kwamba kila mmoja wenu atabarikiwa.
Tuesday, October 30, 2012
Natembea na Mungu
"Basi jueni ya kuwa BWANA, Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao na kushika amri zake, hata vizazi elfu." Kum 7:9
Monday, October 29, 2012
Zaburi ya leo
Zaburi 35: 4-5 "Waaibishwe, wafedheheshwe wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma wafadhaishwe wanaonizulia mabaya. Wawe kama makapi mbele ya upepo, Malaika wa Bwana akiwaangusha chini"
Saturday, October 27, 2012
VIFUNGO VYA LAANA
Neno LAANA katika kamusi limetafsiriwa kama ukosefu wa radhi za
mwenyezi Mungu, hasira ya Mungu. Au ni apizo atoalo mtu kwa mtu mwingine ili
afikwe na ubaya, uovu, msiba au hasira ya Mungu. LAANI limetafsiliwa kama, shtakia kwa Mungu, au
ombea uovu.
Zipo laana nyingi lakini leo ningependa kuzungumzia laana
zifuatazo:-
- Ukoo/familia:-
laana zinazojiendeleza kwenye ukoo hutokana na matokeo ama matunda ya
dhambi. Kwa mfano unakuta katika familia husika kuna wengine wana laana za
magonjwa sugu kama kansa, kwenye hiyo hiyo familia wengine hawaolewi,
wengine wameolewa lakini ndoa hazidumu, wengine hawapati mimba. Familia
nyingine utakuta kuna vifo vya ghafla, wanaanza maisha na kufanikiwa na
kuwa na mali na biashara kubwa au kazi lakini mwisho wao wanaishia
kufilisika na kufa kwa mateso makali.Unatakiwa kuomba maombi ya rehema na
toba na lazima utamke kilichofanyika na matokeo yake. Kwa sababu kila dhambi iliyofanyika ni
kutokana na kuwa na miungu mingine. Dhambi inatokea pale mtu anapomwacha
Mungu wa kweli na kusikiliza miungu mingine. Sasa unapokosa msaada wa
Mungu wa kweli unapata misaada ya miungu inayokusababisha wewe kutenda
kinyume na Mungu. “Usiwe na miungu mingine ila Mimi- Kumbukumbu
la torati 5:7”
- Laana
za kulaaniwa na mtu mwingine:- Yawezekana ulikosana na
rafiki yako ama mtu mwingine pengine mwalimu wako wa shule akakuchukia na
kukulaani. Anaweza kukulaani kuwa na kamwe hutakaa uendelee kwa kila
utakalofanya usifanikiwe.
- Laana
za kujilaani mwenyewe:- Kuna watu hawaridhiki na
jinsi walivyo ama niseme viungo vya miili yao, yaani kwa ufupi
hawajikubali ama kujiamini. Utakuta mtu analalamika na kusema “aah mimi
kwa ufupi huu sidhani kama nitakaa nipate mwanamke mrefu atakaenipenda,
ama mwingine atajilaani kwa kusema kamwe hawezi kuwa mtu wa kwanza
darasani kwa sababu tu ya mtu fulani nyumbani kwao hajawahi kuwa” Siku
zote maneno huumba na kujiumba, kwa maana hiyo yale uyatamkayo mdomoni
kwako vivyo hivyo yanafanyika.
- Laana
ya vitu visivyoisha: Kuna watu wamelaaniwa kwa kila
wakigusacho kisiendelee na matokeo yake hujikuta wameanzisha vitu mbali
mbali bila hata kimojawapo kukamilika. Mfano mtu anataka kujenga lakini
anaishia nusu na kuanza kitu kingine ambacho nacho hakifiki mbali. Nataka
kuanzisha biashara ya nguo, atanunua sehemu ya kuuzia nguo lakini hakuna
kitakachoendelea. Watu kama hawa ni wale wanaonena kwa midomo lakini
hawatekelezi.
- Laana ya kufanya tendo la ndoa na dada
yako au kaka yako, baba yako au mama yako
Kuna mambo mengine sio rahisi hata kuelezea lakini yapo na yanafanyika mtu amelala na Dada yake, mwingine na kaka yake, laana ya Mungu imeagizwa juu yao “Kumb 27:22 Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye au Binti ya mamae. Na watu wote waseme Amina”
Haya yote yanatokana na UPOFU wa mawazo. Akili ikifungwa mtu
hawezi kufanya maamuzi yoyote. Pia akili ikifungwa mtu haoni ugumu wa dhambi. “2Wakorintho 3:14 ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana
hata leo hivi wakati lisomwapo Agano la kale, utaji uo huo wakaa, yaani
haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo”. Soma pia Waefeso 4:18
NAVUNJAJE
VIFUNGO?
Biblia inapozungumza habari ya watu waliofungwa wapate
kufunguliwa, hii ina maana ya kuwa kuna watu wamefungwa chini ya utawala wa
nguvu za giza katika ulimwengu wa Roho. Watu hawa wamefungwa kwenye magereza na
Ibilisi.
Tutambue ya kuwa Yesu aliposema amekuja kutuokoa hii inamaanisha
kwamba kuna mahali ambako tusingeweza kujikwamua wenyewe bila nguvu yake yeye
mwenywe kuingia kati yetu.
Aliyahidhirisha haya kwenye kitabu cha nabii Isaya 61:1-2 Roho ya Bwana Mungu i juu yangu kwa sababu Bwana
amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema, amenituma ili kuwaganga
waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za
kufunguliwa kwao”.
Vunja uhusiano wako na hiyo miungu pamoja na kazi zake na agano
lililofanyika kati ya familia au ukoo wako na hiyo miungu. Kila unapotamka
mwisho wake sema kwa sababu nimesamehewa. Ipo mistari mingi ya kuvunja maagano
lakini mimi nitakupa kifungu hiki cha mstari katika kuvunja maagano na mapoozo
ya aina yoyote. “Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo
wake utaondoka begani mwako na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa
kwa sababu ya kutiwa mafuta” Isaya 10:27
Kifungu kingine ambacho waweza tumia ni kwa kutaja maneno haya
wakati wa kuvunja vifungo ama laana “Bwana Yesu, nasimama
mbele zako na katika ulimwengu wa roho, kujiachanisha nafsi yangu (Taja jina
lako) na vifungo vya kuzimu kwa upande wa baba yangu na mama yangu kwa sababu
nimesamehewa.” Endelea vivyo hivyo kwa kutaja, roho na mwili kwa kutumia
maneno hayo hayo uponyaji hufanyika katika nafsi, mwili na roho.
Mtegemee Roho
Mtakatifu kwa maana atakufundisha mengi ikiwemo kuomba na maagizo ya Yesu. Na
kwa kufuata maagizo ya Yesu na kuenenda kwa roho hivyo vifungo vya nafsi
vitakwisha. Soma Wagalatia 5:16-25, Luka 22:40-46. Kudumu katika maombi,
kuenenda kiroho na kuepuka uovu ni muhimu kwa sababu kwa kufuata misingi hiyo
ndipo unafunguliwa vifungo kwa kuombewa ama kwa nguvu inayotenda kazi ndani
yako kupitioa roho mtakatifu. Lakini pia ni muhimu kujua ya kwamba sala ya toba
pekee haitoshi kumfungua mtu kama ana vifungo na sio imani tu bali na juhudi
binafsi ya mtu itasaidia katika kumuweka huru. Wapo watu wanaotaka kupokea
miujiza bila ya kuwa na mabadiliko yoyote, ama bila kusoma neno la Mungu na
kukua kiroho ama bila kuomba. Wao husubiria siku za maombi, ama mikesha ama
makongamano ya maombi ili waombewe kisha baada ya hapo hawajishughulishi katika
kukua kiimani.
Kuwa hodari
katika Bwana ili upate ulinzi wa Mungu. Waefeso 6:10-11 Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa
nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu mpate kuweza kuzipinga hila za shetani”
Maana ya kuwa
hodari katika Bwana ni kukaa kwenye maombi, kusoma na kulishika neno lake liwe
ndani yako, na kutaka kumjua yeye zaidi. Sikuzote Sali kwa bidii katika
kupambana na muovu shetani ndo mana tunaambiwa vaeni silaha zote za Mungu ili
kuweza kupingana na hila za muovu shetani.
Mbarikiwe na
Mungu!
Thursday, October 25, 2012
Mngoje Bwana!
"Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja wala hatakawia. Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani, naye akisita-sita roho yangu haina furaha naye" Waebrania 10:37-38
Wednesday, October 24, 2012
Mwaka wa Bwana uliokubaliwa!
"Roho ya Bwana Mungu i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema, amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo kuwatangazia mateka uhuru wao na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao" Isaya 61:1
Kipekee ni neno ambalo nikisoma nafarijika na kutambua kuwa Bwana wetu yupo sikuzote kutufuta machozi na ni tumaini la wengi waliokata tamaa. Neno hili linasema kwamba wote waliao watafarijika na kupewa taji la maua, mafuta ya furaha badala ya maombolezo na vazi la sifa badala ya roho nzito na vivyo hivyo wataitwa miti ya haki iliyopandwa na Bwana ili atukuzwe.
Yamkini unapitia mambo magumu pasipo wewe kuona njia, jua ya kuwa Mungu anaskia kilio chako. Pengine huu sio mwaka wako, lakini jua muda wako hauko mbali. Mwamini Mungu na kumtegemea kila siku. Muombe Mungu akuzidishie Imani yako katika kumwamini yeye kuwa ndiyo muweza wa kila kitu na anajibu maombi.
Mungu awabariki!
Kipekee ni neno ambalo nikisoma nafarijika na kutambua kuwa Bwana wetu yupo sikuzote kutufuta machozi na ni tumaini la wengi waliokata tamaa. Neno hili linasema kwamba wote waliao watafarijika na kupewa taji la maua, mafuta ya furaha badala ya maombolezo na vazi la sifa badala ya roho nzito na vivyo hivyo wataitwa miti ya haki iliyopandwa na Bwana ili atukuzwe.
Yamkini unapitia mambo magumu pasipo wewe kuona njia, jua ya kuwa Mungu anaskia kilio chako. Pengine huu sio mwaka wako, lakini jua muda wako hauko mbali. Mwamini Mungu na kumtegemea kila siku. Muombe Mungu akuzidishie Imani yako katika kumwamini yeye kuwa ndiyo muweza wa kila kitu na anajibu maombi.
Mungu awabariki!
Tuesday, October 23, 2012
Zaburi ya Leo
Zaburi 92:1-2 "Ni neno jema kumshukuru Bwana, na kuliimba jina lako Ee uliye juu. Kutangaza rehema zako asubuhi, na uaminifu wako wakati wa usiku"
Sunday, October 21, 2012
NI NEEMA PEKEE HUTUOKOA
Matendo hayatuokoi bali neema hutuokoa. Mungu pekee ndiye
atakayetuokoa na hivyo basi haina budi umkiri na kumwamini ndiyo wokovu
unaingia halafu matendo yanafuata. “Basi ni vivi hivi
wakati huu wa sasa yako mabaki waliochaguliwa kwa neema. Lakini ikiwa ni kwa
neema, haiwi kwa matendo tena au hapo neema isingekuwa neema.” Warumi 11:5-6
Yakupasa kuufanyia kazi wokovu wako ili upate neema kutoka kwa
Bwana Yesu. Katika maandiko matakatifu anatuasa ya kuwa tutimize wokovu wetu
wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. “Basi, wapendwa
wangu kama vile mlivyotii sikuzote si wakati mimi nilipokuwa tu, bali sasa
zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na
kutetemeka” Wafilipi 2:12
Katika kufanya yote haya yakupasa kumfuata Yesu na kuwa
mwanafunzi wake.Je sifa zipi zinamuonyesha mtu kuwa mwanafunzi wake? Yakupasa
kutoa maisha yako na kumtumikia Yesu, Lazima uwe mfuasi wake yaani unaenda pale
Yesu anataka uende, unafanya yale ambayo yeye anataka ufanye na sifa nyingine
ni kujifunza zaidi kufanana na yeye. Unahitaji kuubeba msalaba katika hatua za
kutaka kufanana na Yesu.
Hatua
za kubeba Msalaba/ Bearing a cross
·
Jikubali (Accept
who you are and don’t live in denial)- Kama
hujajikubali ulivyo huwezi kufunction vile ambavyo unafikiri ungefunction.
Usijaribu kuwa mtu fulani, jikubali ulivyo. Kwa maana tumeumbwa kwa sura na
mfano wa Mungu. “Kabla sijakuumba katika tumbo
nalikujua na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa, nimekuweka kuwa nabii wa
mataifa”Yeremia 1:5
Kuna watu huwa wanasumbuliwa na
vitu vidogo sana katika maisha yao. Unaweza kuta mtu hana raha analalamika yani
Mungu sijui kwa nini kaniumba hivi? Ukimuuliza tatizo ni nini anaweza kukujibu
kuwa sijui kwa nini mimi mweusi sana, mimi nina tako kubwa ama sina matako
kabisa au sina nywele, mwingine atakulalamikia ana matiti makubwa ama hana
kabisa. Ukiangalia wenzetu huku nchi zilizoendelea wanafanya vituko kweli.
Kutwa kwenda kwa madaktari kuongeza/kupunguza matiti, kuchoma sindano za midomo
iwe mikubwa na Kubadili jinsia na mambo mengine kama hayo. Na siku zote
mwanadamu haridhiki na chochote kwa sababu wengine baada ya kufanya vitu kama
hivyo nilivyotaja hapo juu bado wataona kuna kasoro nyingine na hivyo watataka
kubadilisha sehemu za miili yao tena na tena. Mshukuru Mungu kwa jinsi ya alivyokuumba
kwa sababu katika macho yake hakuna mtu aliye mbaya kwake. “ Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya
kutisha. Matendo yako ni ya ajabu. Na nafsi yangu yajua sana” Zaburi 139:14
·
Eneo lako
ni lipi?- Lazima kukubali jaribu lako na kulifanyia kazi- Pengine jaribu
lako ni kukosa mtoto ama kazi, kukosa mchumba. Yakupasa kulifanyia kazi na
kumuomba Mungu akuondolee ile tabia ya kulalamika zaidi akupe maarifa ya
kulifanyia kazi jaribu lako. Kamwe usijilinganishe na mtu kwamba kwa nini huyu
ana hiki na mimi sina, kwa nini yeye amepata mapema nami sijapata ili hali
nimeomba muda mrefu na vitu kama hivyo. Mungu hana upendeleo na mawazo anayotuwazia
ni mema. Ukiendelea kuwa muaminifu kwake atakupenda daima. Jua muujiza wako uko
mlangoni kwako Mungu anakusubiria ufungue mlango na uupokee. Hivyo basi ni
vyema sikuzote kujiweka mtu mwenye furaha na amani ndani ya moyo wako. Mara
nyingi tunalalamika pasipo kujua kwamba tunajiondolea baraka zetu wenyewe.
Lijue jaribu lako na fanya kazi ya kuliombea bila kutia moyo wa mashaka.
·
Kubali
jaribu lako unalopitia kwa wakati sijui kama Kiswahili imekaa sawa lakini kwa
lugha ingine ni Embrace the walk- He never promised that the walk
will be easy. Hakusema kila kitu kitakuwa mteremko bali ni kujibiidisha katika
kumtumikia yeye. Siku zote mtu akiomba kuna majibu matatu (1) HAPANA (2) NDIYO
lakini SUBIRI (3) NDIYO WAKATI NI SASA. Vita ni vingi sana hasa katika kumtafuta Mungu.
Mpaka uuone mkono wake lazima kuna kupitia dhoruba nyingi. Kila jaribu
linalokujia Mungu atakuonyesha mlango wa kutokea. Do not blame your past just
make the most of it. Chochote ulichopitia nyuma usikilalamikie kwa sababu huo
ni mtaji wako, it’s your unique story. Likumbatie jaribu lako lililokupata na
kulifanyia kazi. Mfano mzuri ni Oprah, she was abused and she used that to tell
stories. Ndo mana nasema that was her profit and she made the most out of it,
look where she is now. Jaribu upitalo is not to break you but to make you. Tena
Mungu hapendi watu wanaolalamika yaani wao siku zote kwao ni mbaya ama mambo
yao hayaendi kama wanavyotaka.
Ndo mana wazungu wanasema “When the going gets tough, the tough gets
going”. Kabla hujafikia malengo unayotaka kufikia lazima upitie misuko suko
mingi ambayo hiyo ndiyo inakujenga. You are building muscles of your life, acha
kulalamika na mtumikie Mungu.
Mungu awabariki!
Subscribe to:
Posts (Atom)