Sunday, October 21, 2012

NI NEEMA PEKEE HUTUOKOA


Matendo hayatuokoi bali neema hutuokoa. Mungu pekee ndiye atakayetuokoa na hivyo basi haina budi umkiri na kumwamini ndiyo wokovu unaingia halafu matendo yanafuata. “Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa yako mabaki waliochaguliwa kwa neema. Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena au hapo neema isingekuwa neema.” Warumi 11:5-6

Yakupasa kuufanyia kazi wokovu wako ili upate neema kutoka kwa Bwana Yesu. Katika maandiko matakatifu anatuasa ya kuwa tutimize wokovu wetu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka. “Basi, wapendwa wangu kama vile mlivyotii sikuzote si wakati mimi nilipokuwa tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka” Wafilipi 2:12

Katika kufanya yote haya yakupasa kumfuata Yesu na kuwa mwanafunzi wake.Je sifa zipi zinamuonyesha mtu kuwa mwanafunzi wake? Yakupasa kutoa maisha yako na kumtumikia Yesu, Lazima uwe mfuasi wake yaani unaenda pale Yesu anataka uende, unafanya yale ambayo yeye anataka ufanye na sifa nyingine ni kujifunza zaidi kufanana na yeye. Unahitaji kuubeba msalaba katika hatua za kutaka kufanana na Yesu.

Hatua za kubeba Msalaba/ Bearing a cross

·        Jikubali (Accept who you are and don’t live in denial)-  Kama hujajikubali ulivyo huwezi kufunction vile ambavyo unafikiri ungefunction. Usijaribu kuwa mtu fulani, jikubali ulivyo. Kwa maana tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua na kabla hujatoka tumboni nalikutakasa, nimekuweka kuwa nabii wa mataifa”Yeremia 1:5

Kuna watu huwa wanasumbuliwa na vitu vidogo sana katika maisha yao. Unaweza kuta mtu hana raha analalamika yani Mungu sijui kwa nini kaniumba hivi? Ukimuuliza tatizo ni nini anaweza kukujibu kuwa sijui kwa nini mimi mweusi sana, mimi nina tako kubwa ama sina matako kabisa au sina nywele, mwingine atakulalamikia ana matiti makubwa ama hana kabisa. Ukiangalia wenzetu huku nchi zilizoendelea wanafanya vituko kweli. Kutwa kwenda kwa madaktari kuongeza/kupunguza matiti, kuchoma sindano za midomo iwe mikubwa na Kubadili jinsia na mambo mengine kama hayo. Na siku zote mwanadamu haridhiki na chochote kwa sababu wengine baada ya kufanya vitu kama hivyo nilivyotaja hapo juu bado wataona kuna kasoro nyingine na hivyo watataka kubadilisha sehemu za miili yao tena na tena. Mshukuru Mungu kwa jinsi ya alivyokuumba kwa sababu katika macho yake hakuna mtu aliye mbaya kwake. “ Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu. Na nafsi yangu yajua sana” Zaburi 139:14

·        Eneo lako ni lipi?- Lazima kukubali jaribu lako na kulifanyia kazi- Pengine jaribu lako ni kukosa mtoto ama kazi, kukosa mchumba. Yakupasa kulifanyia kazi na kumuomba Mungu akuondolee ile tabia ya kulalamika zaidi akupe maarifa ya kulifanyia kazi jaribu lako. Kamwe usijilinganishe na mtu kwamba kwa nini huyu ana hiki na mimi sina, kwa nini yeye amepata mapema nami sijapata ili hali nimeomba muda mrefu na vitu kama hivyo. Mungu hana upendeleo na mawazo anayotuwazia ni mema. Ukiendelea kuwa muaminifu kwake atakupenda daima. Jua muujiza wako uko mlangoni kwako Mungu anakusubiria ufungue mlango na uupokee. Hivyo basi ni vyema sikuzote kujiweka mtu mwenye furaha na amani ndani ya moyo wako. Mara nyingi tunalalamika pasipo kujua kwamba tunajiondolea baraka zetu wenyewe. Lijue jaribu lako na fanya kazi ya kuliombea bila kutia moyo wa mashaka.

·        Kubali jaribu lako unalopitia kwa wakati sijui kama Kiswahili imekaa sawa lakini kwa lugha ingine ni Embrace the walk- He never promised that the walk will be easy. Hakusema kila kitu kitakuwa mteremko bali ni kujibiidisha katika kumtumikia yeye. Siku zote mtu akiomba kuna majibu matatu (1) HAPANA (2) NDIYO lakini SUBIRI (3) NDIYO WAKATI NI SASA. Vita ni vingi sana hasa katika kumtafuta Mungu. Mpaka uuone mkono wake lazima kuna kupitia dhoruba nyingi. Kila jaribu linalokujia Mungu atakuonyesha mlango wa kutokea. Do not blame your past just make the most of it. Chochote ulichopitia nyuma usikilalamikie kwa sababu huo ni mtaji wako, it’s your unique story. Likumbatie jaribu lako lililokupata na kulifanyia kazi. Mfano mzuri ni Oprah, she was abused and she used that to tell stories. Ndo mana nasema that was her profit and she made the most out of it, look where she is now. Jaribu upitalo is not to break you but to make you. Tena Mungu hapendi watu wanaolalamika yaani wao siku zote kwao ni mbaya ama mambo yao hayaendi kama wanavyotaka.

Ndo mana wazungu wanasema “When the going gets tough, the tough gets going”. Kabla hujafikia malengo unayotaka kufikia lazima upitie misuko suko mingi ambayo hiyo ndiyo inakujenga. You are building muscles of your life, acha kulalamika na mtumikie Mungu.

Mungu awabariki!

2 comments:

  1. Ninapitia jaribu la kuwa na binti ambaye anaipenda dunia na mambo yake kama vile kuwa msanii na kuvaa mavazi ya aibu pamoja na unzinzi wa kutisha kwa kweli nina mpenda binti yangu lakini mambo anayofanya ninayachukia muniombee niwe na uvumilivu ile twende sote kwa BABA.

    ReplyDelete
  2. Pole sana ndugu yangu. Mungu wetu ni mwema na anasikia maombi yetu. Nakushauri usikate tamaa hata kidogo bali endelea kumkabidhi kwa Mungu. Mwombe amfunike kwa damu ya mwana wake mpendwa Yesu Kristo. Huo ni moja ya mitihani ambayo Mungu hutujaribu nayo, nina Imani binti ataacha mambo hayo yote ya dunia. Nashukuru kwa kushare nasi, tutakuweka kwenye maombi yetu.
    Ubarikiwe sana!

    ReplyDelete