Wednesday, October 24, 2012

Mwaka wa Bwana uliokubaliwa!

"Roho ya Bwana Mungu i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema, amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo kuwatangazia mateka uhuru wao na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao" Isaya 61:1

Kipekee ni neno ambalo nikisoma nafarijika na kutambua kuwa Bwana wetu yupo sikuzote kutufuta machozi na ni tumaini la wengi waliokata tamaa. Neno hili linasema kwamba wote waliao watafarijika na kupewa taji la maua, mafuta ya furaha badala ya maombolezo na vazi la sifa badala ya roho nzito na vivyo hivyo wataitwa miti ya haki iliyopandwa na Bwana ili atukuzwe.
Yamkini unapitia mambo magumu pasipo wewe kuona njia, jua ya kuwa Mungu anaskia kilio chako. Pengine huu sio mwaka wako, lakini jua muda wako hauko mbali. Mwamini Mungu na kumtegemea kila siku. Muombe Mungu akuzidishie Imani yako katika kumwamini yeye kuwa ndiyo muweza wa kila kitu na anajibu maombi.

Mungu awabariki!

No comments:

Post a Comment