“Amka Amka jivike nguvu zako Ee Sayuni; jivike Mavazi yako
mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako
asiyetahiriwa wala aliye najisi, jikung’ute mavumbi uondoke, uketi ee
Yerusalem. Jifungulie vifungo vya shingo yako Ee Binti Sayuni uliyefungwa”
Isaya 52:1-2
MAANA YAKE: Unapoamua
kufuata mwelekeo mpya wa maisha unatakiwa kuwa tayari kuacha mambo ya zamani
yanayokuzuia. Kwa maana umepewa tohara ya moyo kwa kuokolewa. Kama wewe ni
mfanyabiashara uachane na vitu ambavyo vinakurudisha nyuma na kukukwamisha.Kama
maisha yako yalikuwa ya starehe kabla ya biashara, basi yakupasa kufikiria zaid
jinsi ya kupunguza matumizi yako katika starehe pindi umekuwa na biashara yako
na unataka maendeleo. Think out of the box kwamba nini kitafanya biashara yako
ikue. Pengine ulikuwa mtu wa kusema watu, mchonganishi kama umeamua kumfuata Yesu achana na hivyo vitu na jitenge kabisa na watu wanaopenda mambo kama hayo. Jikung'ute nguo zako na usonge mbele. Usijali watu watakuonaje ama kukusemaje, mfuate Mungu pekee ndo rafiki wa kweli.
Naupenda sana huu wimbo
ReplyDelete