Marko 11:25-26, Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. [Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]
TAFAKARI: Kuna maombi mengi katika maisha ya
wakristo hayajibiwi sio kwa sababu ya dhambi au shetani ana nguvu sana bali ni
kwa sababu kuwa wengi hawajasemehe. Kuna wengi wetu tunaishi na vinyongo vya
watu ndani mwetu, tuna mengi tumeyabeba na kuna uchungu wa mambo mengi ambao
hatutaki kuachilia. Hii imepelekea maombi yetu kutojibiwa maana kutosamehe ni
jambo mojawapo inayopelekea kutojibiwa maombi. Samahe leo hii.
SALA : Mungu wangu na Baba yangu, naomba unipe neema
ya kusamehe na kuachilia katika maisha yangu. Nisadie nisamehe hata yale ambayo
vidonda vyake bado vibichi mpaka leo ili na wewe upate kunisamehe. Kwa Jina la Yesu,
Amina.
No comments:
Post a Comment