TAFAKARI: Mngoje
Bwana kwa matumaini makubwa kwa maana siku zi karibu kama anenavyo kwenye
maandiko yake matakatifu. Kama utakuwa ni mtu mwenye imani haba, Mungu hatakuwa na furaha juu yako.
SALA: Mwenyezi Mungu nasema
asante kwa maisha haya uliyonipa. Bwana naomba ukanizidishie imani ndani ya
moyo wangu nikungoje wewe bila kuchoka, nijaze roho wako mtakatifu aliye
msaidizi wa kila aliye mwaminifu ili imani yangu isitereleke. Naomba na kupokea katika
jina la Yesu, Amen.Karibuni katika blog hii, mahali ambapo utajifunza kuishi na kuenenda katika njia ya Kikristo na kusaidiana kukua kiroho kwa kusoma na kufundishana neno la Mungu. Ni matumaini yangu kwamba kila mmoja wenu atabarikiwa.
Friday, February 8, 2013
Neno la leo
Ebr 10:37-38 “Kwa kuwa
bado kitambo kidogo sana, yeye ajaye atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye
haki wangu ataishi kwa imani; naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye”
Thursday, February 7, 2013
Neno la leo
Gal 5:5 “Maana sisi wa roho
tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani”
TAFAKARI: Pengine wewe ni mwenye imani haba, muombe Mungu
akuongoze katika haki ili uweze kulifikia tumaini jema.Ukiwa unaamini hakika mambo yako mengi yatakuendea vyema.
SALA: Niseme nini Bwana
zaidi ya kushangaa makuu yako mengi,na umeniwezesha katika kufikia malengo
yangu mengi. Bwana hata pale ninapokutana na vikwazo vingi, naomba uendelee
kunipigania zaidi nikawe mwenye misimamo na kutokata tamaa. Niimarishe katika kukuamini wewe Bwana kwa maana kwako tu ndo kuna tumaini jema.Naomba na kupokea,
Amen.Wednesday, February 6, 2013
Neno la leo
Ebr 4:13 “Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele
zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo
yetu”
TAFAKARI: Hakuna kitu ambacho Mungu hawezi kuona kwa
mwanadamu. Wakati mwingine mtu anaweza kutenda jambo la kikatili asijue ya
kwamba Mungu anamuona, ila tambua ya kwamba Mungu anaona kila mahali.
SALA: Mungu baba, nakuja kwako kwa unyenyekevu
nikiomba unisamehe dhambi nilizotenda ambazo machoni pa wanadamu hazifahamiki
bali wewe wazitambua. Naomba uniweke huru kwa damu yako ya thamani, katika jina
la Yesu naomba na kupokea, Amen.Tuesday, February 5, 2013
Neno la leo
Tito 2:11-12 “Maana
neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa
ubaya na tamaa za kidunia; na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa”
TAFAKARI: Katika misemo ya kawaida kwa maisha yetu tunaposema kitu kumefunuliwa basi jua kina uwezo wa kufunikwa. Mungu ametoa neema kwa wanadamu wote kwa kutupa uhai na hivyo yatupasa kutenda mema, kwa maana ipo siku neema itafungwa na tumeshindwa kutimiza wajibu wetu kwa wakati tuliopewa hakika tutalia.
TAFAKARI: Katika misemo ya kawaida kwa maisha yetu tunaposema kitu kumefunuliwa basi jua kina uwezo wa kufunikwa. Mungu ametoa neema kwa wanadamu wote kwa kutupa uhai na hivyo yatupasa kutenda mema, kwa maana ipo siku neema itafungwa na tumeshindwa kutimiza wajibu wetu kwa wakati tuliopewa hakika tutalia.
SALA: Mwenyezi Mungu asante
kwa maana umenipa neema kuu machoni pangu. Nipe akili ya kutoweza kuichezea
neema hii uliyonipa bure, niwezeshe katika muda wangu huu wa kuishi nikutumikie
wewe daima.Naomba na kupokea katika jina la Kristo Yesu, Amen.
Monday, February 4, 2013
Neno la leo
Luka 11:28 “Lakini
yeye alisema afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika,”
TAFAKARI: Imetupasa kumwogopa Mungu na kumheshimu,na tusiwakasirishe wazazi wetu, ila tuwatumikie, tuwatii na kuwapenda kwa moyo wote.
SALA: Mwenyezi Mungu, asante kwa upendo wako kwangu, Wewe uliye mzazi wangu wa kwanza nakupenda na naliheshimu neno lako, niwezeshe nizidi kuwaheshimu wazazi wangu ulionipa wewe na wakubwa wangu, katika jina la Yesu naomba na kupokea, Amen.
TAFAKARI: Imetupasa kumwogopa Mungu na kumheshimu,na tusiwakasirishe wazazi wetu, ila tuwatumikie, tuwatii na kuwapenda kwa moyo wote.
SALA: Mwenyezi Mungu, asante kwa upendo wako kwangu, Wewe uliye mzazi wangu wa kwanza nakupenda na naliheshimu neno lako, niwezeshe nizidi kuwaheshimu wazazi wangu ulionipa wewe na wakubwa wangu, katika jina la Yesu naomba na kupokea, Amen.
Friday, February 1, 2013
Neno la leo
Zaburi 63:3 “Maana
fadhili zako ni njema kuliko uhai; midomo yangu itakusifu”
TAFAKARI: Fadhili
za Bwana ni za milele na hivyo hatuna budi kulitangaza jina lake na kumsifu
yeye daima.
SALA: Kitu ninachokipenda
katika maisha haya ni mifano ya uzuri wako, wewe utendaye miujiza mikuu siwezi
kamwe kuwa na mashaka nawe. Naomba nikuimbie nyimbo za kukusifu na kukuinua
wewe Mungu, zaidi ndimi zangu ziinue jina lako Bwana kwa maana hakuna kitu
chochote kizuri kitakachoshindana na upendo wako. Katika jina la Yesu naomba na
kushukuru, Amen.Thursday, January 31, 2013
Neno la leo
Yeremia 5:23 “Lakini
watu hawa wana moyo wa kuasi na ukaidi; wameasi, wamekwenda zao”
TAFAKARI: Moyo wa
kuasi na wenye ukaidi humtenga mtu asiwe karibu na Mungu.
SALA: Mungu wewe uchunguzaye moyo wa kila mtu na kujua tabia zao naomba
nimulike Mungu wangu kwa taa yako, nakiri kwamba natakiwa niache tabia yangu
hii mbaya, ni nani wa kuniweka huru kama sio wewe Bwana wangu? Niondolee ukaidi
ndani ya moyo wangu na zaidi unitenge na maovu mengi ya dunia hii.Asante Bwana
kwa maana umeniweka huru. Naomba na kupokea katika jina la Yesu kristo, Amen
Subscribe to:
Posts (Atom)